Subscribe:

Pages

Featured Posts

Saturday, May 26, 2012

MISS DAR INTER COLLEGE KURINDIMA JUNI 8 CLUB SUNCIRO


SHINDANO la kumsaka Miss Dar Intercollege 2012 linatarajiwa kufanyika Juni 8 kwenye ukumbi wa Sunciro, ulipo Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam, imefahamika.

Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba warembo watakaoshiriki shindano hilo wanaendeleza na mazoezi kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na Bob Rich.

Alisema mpaka sasa warembo 12 kutoka vyuo vyaBiashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamesharipoti kambini.

Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Hilda Edward, Nancy Maganga, Saada Seleman, Neema Nashon, Rose Muchunguzi, Fina Revocatus,Jane Augustino,Theresia Issaya na Natasha Deo.Taji la kitongoji hicho linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.

Kwa upande mwingine, mratibu huyo ameyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake na hasa ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya juu.

“Tunaomba makampuni mbalimbali yajitokeze kudhamini shindano letu…mpaka sasa wadhamini tulionao ni pamoja na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, Dodoma Wine na Clouds Fm.

TAIFA STARS, MALAWI ZATOKA SULUHU.

Haruna Moshi akionyesha makeke yake langoni mwa timu ya Malawi katika mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam..
 Mshambuliaji wa Timu ya Taifa Stars,Haruna Moshi "Boban" akiwachachafya mabeki wa timu ya Malawi katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Hatari langoni mwa timu ya Malawi.........
 Mchambuliaji wa Timu ya Taifa,Mbwana Samatta akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Malawi,Limbikani Mzava katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kipindi cha cha mchezo huu kimemalizika huku timu zote mbili zikitoka bila kufungana.
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakitoka uwanja baada ya kumalizika kwa Mchezo huo.
 Taifa Stars wala Malawi hakuna aliefanikiwa kupata goli, hata hivyo wamalawi wameshambulia mara nyingi katika lango la Taifa Stars katika kipindi cha kwanza, lakini uimara wa mabeki pamoja na Golikipa Juma Kaseja umesaidia sana Taifa stars kutofungwa , Taifa Stars yenyewe imefanya mashambulizi ya hatari,hata hivyo haikuwa bahati yao ambapo mpaka mwisho wa mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 0-0.

Timu ya Malawi iko safarini kuelekea nchini Uganda ambako itacheza na timu ya Uganda Cranes.

TAASISI YA WANAFUNZI WANAOSOMA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOMSSO) YAPATA VIONGOZI WAPYA LEO MCHANA

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kutoka Mwaka wa 1 alipokua akitoa maelekezo ya nini kifanyike kabla ya Zoezi la Kupiga kura na Kutangaza washindi
 Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti katika taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Edgar Kelvin ambaye anasomma mwaka wa 2 alipokua akinadi sera zake kabla zoezi la kupiga alijaanza
Mgombea wa pili wa nafasi ya Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bi Loyce Haule ambaye anasoma mwaka wa 2 akinadi Sera zake
Mgombea wa Tatu wa Nafasi ya Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Mwakindaga Emmanuel ambaye anasoma mwaka wa 2 akinadi sera zake
Mgombea Wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Mtono Juma ambaye amepita bila kupingwa kutoka na kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo na ni mwanafunzi kutoka mwaka wa kwanza
Mmoja wa Wanafunzi Kutoka Mwaka wa 3 Sophia Mkingiye akiuliza Maswala mara baada ya Wagombea kumaliza kunadi sera wakati walipokua wakiomba kura kwa wajumbe na wanachama
Mwanafunzi wa Mwaka wa 2 ambaye anasoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Bi Hadija Hassan alipokua akiuliza swali wakati kwa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakati Wa Uchaguzi wa Kuwachagua Viongozi wapya wa Nafasi mbalimbali Katika Taasisi hiyo Mchana wa Leo
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma waliohudhuria katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wa taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) katika uchaguzi uliofanyika ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma mchana wa leo
Zoezi la Kuesabu kura likiendelea hapo 
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bw Emmanuel Misungwi Alipokua akitoa Shukrani wa wanachama na wadau wa taasisi hiyo Kwa Kipindi Chote alichokua madarakani kwa mazuri na mabaya ambayo taasisi imepitia na kushukuru kwa wanachama kushiriki zoezi la kupiga kura na kupata viongozi wapya wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)
Baadhi ya Viongozi wapya wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waliomaliza muda wao leo mara baada ya zoezi la kupiga kura kumalizika na hatimaye kuwapata viongozi wa taasisi ya wanafunzi wanasoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma mchana wa leo
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma aliyemaliza muda wake leo Mh Emmanuel Misungwi (Katikati) Akiwa katika Picha ya Pamoja na Mwenyekiti mpya wa Taasisi hiyo Mh Edgar Kelvin (Wa kwanza kulia) na Aliyekuwa Mwenyekiti Wa UChaguzi Wa Kwanza Kushoto.

MAMA ASHA BILAL AKIZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI BOTSWANA

 Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal akizungumza na Watanzania wanaishi Nchini Botswana leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu wa Rais wa For Conervation Policy kulia na Waziri wa Fedha wa Kenya Mhe. Robinson Njeru baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku mbili kwa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu maendeleo endelevu kwa nchi za bara la Afrika uliomalizika mjini Gaborone. Botswana leo jioni.
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamojan a Watanzania wanaoishi nchini Botswana baada ya kuzungumza na Watanzania hao leo jioni mjini Gaborone Botswana.

FINA REVOCATUS AIBUKA MSHINDI WA REDD'S MISSS IFM 2012

 
Washiriki walioingia kwenye tano Bora.
Mshindi wa Redd's Miss IFM 2012,Fina Revocatus (katikati) akiwa na Mshindi wa Pili,Jane Augustino (kushoto) na wa Tatu Theresia Issaya muda mfupi baada ya kumalizika kwa shindano lao hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Jijini Dar.
 
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Diamond akifanya vitu vyake wakati wa onyesho hilo la urembo  lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Peal,Ubungo Jijini Dar.

Friday, May 25, 2012

TANZANIA BEGA KWA BEGA NA UNDP KUJENGA AFRIKA YENYE UHAKIKA WA CHAKULA.

 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou akizungumza kwa niaba ya UNDP kuhusiana na kuzinduliwa kwa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 ambapo amesema huu sasa ni wakati kwa nchi za Afrika haswa zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara kujenga mazingira ya kuelekea mustakabali wenye uhakika wa chakula.
 Mshauri wa Uchumi UNDP Bw.Amarakoon Bandara akifanya 'presentation' ya Ripoti hiyo. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poinsot.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou (kulia) wakifuatilia maoni ya Uchambuzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kutoka kwa Maprofesa wa Vyuo vikuu nchini.
 Dr. John Mduma akifanya majumuisho ya nini kifanyike kukabiliana matatizo ya uhaba wa chakula yanayolikabili bara la Afrika na Afrika Mashariki.
Profesa Joyce Kinabo wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine akieleza uhifadhi wa Chakula kwa ajili ya matumizi ya baadae
Baadhi ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wadau wa Serikali wakichangia maoni yao kuhusiana na Ripoti hiyo.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) akisoma hotuba wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poinsot.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Mbene (MB) akikata utepe kuzindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou.
 "Sasa imezinduliwa rasmi" Mgeni rasmi Mh. Janet Mbene na Dk. Alberic Kacou wakionyesha Ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakipitia Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 kuelekea kwenye Mustakabali wenye uhakika wa Chakula kwa nchi za Afrika iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam

Bara la Afrika ikiwemo Tanzania limeshakumbwa na matukio kadhaa ya kukabiliwa na uhaba wa chakula, uliokwenda sambamba na matukio ya watu wengi kupoteza maisha haswa Kusini mwa jangwa la Sahara na Ukanda wa Sahel eneo la Afrika Magharibi.

Hali hiyo imekuwa moja ya changamoto kubwa inazozikabili serikali za mataifa hayo ambapo yanapambana ili kuitatua ili kila mwananchi barani Afrika aweze kufurahia kukua kwa uchumi.

Akitoa hotuba wakati akizindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2012 leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Janet Membe (MB) amesema kwa muda mrefu sura ya eneo la nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara imekuwa ni ya njaa ya kukithiri, ambapo zaidi ya mtu mmoja katika kila waafrika wane wana tatizo la upungufu wa lishe.

Amesema Ripoti hiyo inaonyesha kuwa pamoja na ukweli kwamba baadhi ya nchi zinazokuwa kwa kasi kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi ziko Afrika, lakini bado hali ya maisha ya waafrika ni duni.

Awali Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa UNDP nchini Tanzania Dk. Alberic Kacou alisema bara la Afrika limejaliwa kuwa na ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha na hali nzuri ya hewa kwa kukuzia mazao, lakini swali la kujiuliza ni kwanini bado kuna uhaba wa chakula.

Hata hivyo Dk. Kacou ametoa matumaini kuwa bara la Afrika bado lina uwezo wa kujijengea mazingira ya kuwa na akiba ya kutosha ya chakula kwa kipindi kijacho.

Ripoti hii ya Kwanza ya Maendeleo ya Afrika inasema kwamba ongezeko endelevu katika uzalishaji kwenye kilimo kunalinda haki ya chakula na uwezo wa watu kupata chakula.

MAMBO YANAYOENDELEA NDANI YA YANGA

Kwa vile wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji ya Yanga akiwemo Mwenyekiti wa kamati hiyo Lloyd Nchunga wamejiuzulu, Kamati ya Uchaguzi ya Yanga imeliandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka mwongozo juu ya hilo.

 Kwa kuzingatia hilo, TFF imepeleka suala hilo kwa kamati yake ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ili itoe maoni yake kisheria ya nini kinafanyike kuhakikisha Yanga inaendelea na shughuli zake kama kawaida.

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana leo jioni kushughulikia suala hilo na baadaye Kamati ya Uchaguzi ya Yanga pamoja na Kamati ya Uchaguzi ya TFF zitapewa maelekezo ya kufanya kwa kuzingatia taratibu zilizopo.

 ASHANTI, POLISI KUFUNGUA LIGI YA TAIFA
Michuano ya Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa inaanza Mei 27 mwaka huu katika vituo vitatu tofauti huku Ashanti United ya Ilala na Polisi ya Mara zikifungua dimba katika Kituo cha Musoma.

 Ligi hiyo ambayo inatarajia kumalizika Juni 12 na 13 mwaka huu itashuhudia mechi mbili kwa siku katika kila kituo, huku ya kwanza ikichezwa saa 8 mchana na kufuatiwa nay a pili 10 jioni.

 Mechi za ufunguzi Kituo cha Musoma ambapo mechi zake zitachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma ni Flamingo ya Arusha dhidi ya Forest ya Kilimanjaro (saa 8 mchana) wakati saa 10 jioni ni Ashanti United na Polisi.

 Kituo cha Kigoma siku ya ufunguzi kutakuwa na mechi moja tu itakayoanza saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika kati ya Mwadui ya Shinyanga na JKT Kanembwa ya Kigoma. Siku inayofuata ni CDA (Dodoma) vs Majimaji ya Tabora (saa 8 mchana) na Bandari ya Kagera vs Pamba ya Mwanza (saa 10 kamili jioni).

 Tenende ya Mbeya na Kurugenzi ya Iringa ndizo zitakazoanza saa 8 mchana kwenye Kituo cha Mtwara na kufuatia na mechi kati ya Mpanda Stars ya Rukwa na Ndani ya Mtwara kuanzia saa 10 kamili jioni. Mechi hizo zitachezwa katika Uwanja wa Umoja.

TAIFA STARS, MALAWI KUCHEZA KESHO (MEI 26,2012) UWANJA WA TAIFA

Timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) zinapambana kesho (Mei 26 mwaka huu) katika mechi ya kirafiki itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
 
Makocha wa timu zote mbili, Kim Poulsen wa Taifa Stars na Kinnah Phiri wa The Flames wamezungumzia umuhimu wa mechi hiyo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo (Mei 25 mwaka huu) ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
 
Kim ambaye hiyo itakuwa mechi yake ya kwanza tangu asaini mkataba wa kuinoa Stars, amesema baada ya mazoezi ya siku kumi hicho ndicho kipimo chake cha kwanza na cha mwisho kabla ya kucheza na Ivory Coast kwenye mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia itakayofanyika ugenini Juni 2 mwaka huu.
 
“Wachezaji wangu wamekuwa wakipokea mafunzo vizuri ingawa Nurdin Bakari na Thomas Ulimwengu hatakuwepo kwa vile ni majeruhi. Bila shaka baada ya mazoezi ni lazima ujipime, hivyo mechi hii ni muhimu kwangu ukizingatia kuwa kwenye ubora wa viwango vya FIFA, Malawi wako juu yetu,” amesema Kim.
 
Naye Phiri ambaye ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Malawi amesema awali aliombwa mechi na Misri, lakini akaamua kucheza na Taifa Stars kwa vile anaamini kitakuwa kipimo kizuri kwake kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Kenya itakayofanyika Juni 2 mwaka huu jijini Nairobi.
 
“Nimekuja na wachezaji 20 ambapo nusu yao wanacheza mpira wa kulipwa nje ya Malawi, wengi wakiwa Afrika Kusini lakini wapo pia kutoka Msumbiji na mmoja anacheza Hispania katika timu ya vijana ya Atletico Madrid. Tumejianda si kwa mechi hii tu, bali pia dhidi ya Kenya na baadaye Nigeria ambao tutacheza nao numbani Juni 9 mwaka huu,” amesema Phiri ambaye kwenye benchi lake la ufundi anasaidiwa na Young Chimodzi.
 
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa viti vya kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A inayochukua watazamaji 748 tu itakuwa sh. 20,000.

TASWA YAMPONGEZA MHARIRI WA HABARI ZA MICHEZO WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA, TULLO CHAMBO

 
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania(TASWA) kinatoa pongezi kwa Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti la TanzaniaDaima,

Tullo Chambo kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chamacha Riadha Tanzania (RT). Chamboalitwaa nafasi hiyo kwenye Uchaguzi Mkuu wa RT uliofanyika Jumapili mjiniMorogoro, ambapo ni miongoni mwa wajumbe wapya walioingia kwenye chama hicho.

Wenginewalioshinda ni Anthony Mtaka ambaye anakuwa Rais mpya waRT, wakati Makamu wa Rais Utawala ni William Kallaghe, Makamu wa Rais Ufundi,Dk. Ahmed Ndee, Katibu Mkuu, Suleiman

Nyambui, Katibu Msaidizi, Ombeni Zavalla,Mhazini, Is-Haq Suleiman.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mwinga Mwanjala, Meta Petro,Peter Mwita, Rehema Killo, Lwiza John, Zakaria Barrie,
Zakaria Gwanda, RobertKalyahe na Christian Matembo.

TASWAinatambua Chambo ni mwanahabari mzoefu, ambaye kwa muda mrefu amekuwa mhaririwa habari za michezo na ni mtu mwenye kujua mambo mengi yanayohusu riadha,hivyo atakuwa kiungo muhimu kwa watu wa riadha, pia atakuwa kiongo kizuri kwawaandishi wa habari za michezo kuhusiana na mambo ya riadha.

TASWAinaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kadri itakavyoweza na inamtakia kila laheri, huku ikiamini hatawaangusha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa RT waliomuaminiwakamchagua kushika wadhifa huo.

PiaTaswa inawapongeza viongozi wote wa RT walioingia madarakani Jumapili, ikiaminiwatakuwa chachu ya mafanikio ya riadha hapa nchini.

ESRF IKISHIRIKIANA NA OFISI YA RAISI MIPANGO WAENDESHA MKUTANO WA

Mh Profesa Ibrahimu Lipumba ambaye ni Mwenye kiti wa chama cha Cuf na mtalamu wa uchumi wa kimataifa akijadiliana jambo na washiriki wliohuduria mkutano wa kujadili matumizi ya rasilimali  na mgawanyo wapato la taifa katikati ni Profesa Ngila Mwase na bibi Antonina Espiritu(PhD) ambaye ni mtalamu wa wamaswala ya uchumi kutoka shirika la kimataifa la maendeleo la watu wa marekani (USAID) lililopo hapa tanzania picha na chris mfinanga
Baadhi ya wandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo  mkutano huo ulikuwa wa siku moja
Mwenyekiti wa chama cha Cuf na mtalamu wa uchumi wa kima taifa Mh Ibrahimu Lipumba wakiwa na Mbunge wa viti malamu ccm na mwenyekiti wa kamati ya katiba na sheria  Mh Pindi Chana wakimsikiliza Mwenyekiti wa bodi ya ya ushauri wa madini Bwana Richard Kasesela walipokuwa katika mkutano wa uchumi na kujadili mgawanyo wa pato lataifa ulio andaliwa na ESRF na Ofisi ya Rais mipango ulio fanyika katika hoteli ya kilimanjaro dar es salaam picha na chris mfinanga.

Mkutano wa uchumi unao jadili matumizi ya rasilimali na mgawanyo wa pato la taifa  mkutano huo wa siku moja umeshirikisha watalamu mambo ya uchumi wana siasa pamoja na mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao hapa Tanzania.

UZINDUZI WA KAMPENI MPYA YA BIA YA KILIMANJARO IITWAYO 100% TZ FLAVA ILIYO FANYIKA NYUMBANI LOUNGE JIJINI DAR

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Lager,George Kavishe akiwa katika picha ya pamoja na Wacheza filamu,Jacob Steven na Aunt Ezekiel ikiwa ni sehemu ya kampeni hiyo ikiwakilisha Filamu zetu.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Lager,George Kavishe akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa timu ya Simba na Yanga ikiwa ni sehemu ya kampeni mpya ya Bia hiyo inayokwenda kwa jina la 100% Tanzania Flava ikiwakilisha Michezo yetu ambayo imezinduliwa rasmi usiku wa kuamkia leo kwenye kiota cha maraha cha Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam.. 
 MC Ephrahim Kibonde akiongoza shughuli hiyo.
 DJ Peter Moe nae katika safu yake aliinogesha vyema hafla hiyo.
 Mazungumzo ya hapa na pale,Kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Lager,George Kavishe,Mkurugenzi wa  Kiota cha Nyumbani Lounge,G. Habash na Dj Bonventure Kilosa.
 Meneja wa Bia ya Castle Lager,Kabula Nshimo pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Redd's,Victoria Kimaro pia walikuwepo kwenye hafla hiyo.
 Wadau wa TBL. 
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Lager,George Kavishe akiwa katika picha ya pamoja na Wanamuziki Prof. Jay na Janet wa Twanga Pepeta ikiwa ni sehemu ya kampeni hiyo ikiwakilisha Muziki wetu.

Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imezindua Kampeni kubwa ijulikanayo kama 100% TZ Flava yenye kaulimbiu ya ‘Sherekea KilichoChetu’ itakayoendeshwa kwa miezi sita mfulululizo.



Kampeni hiyo ya aina yake inayolenga kuwahamasisha watanzaniakujivunia mambo mbalimbali ya Kitanzania kamavile muziki, lugha na michezo, ilizinduliwa katika Ukumbi wa Nyumbani Lounge.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alizindua penikhiyo akisema kwamba itaendeelea kwa miezi sita kuanzia sasa ikiwa ni mwendelezowa kampeni ya Kili Jivunie uTanzania iliyofanyika mwaka jana kuadhimisha miaka50 ya Uhuru.

Alisema shughuli ya kwanza ilikuwa kuzindua alama ya kampeni hiyo,100% tz Flava- tusherehekee kilicho chetu na nyingine zitafuatia ndani ya miezisita ambapo kampeni hiyo itawafikia watanzania nchi nzima.

“Kampeni hii imeandaliwa kumpa mteja raha, lakini lazima iache ujumbe,ambao ni Sherekea kilicho chetu,”alisema Kavishe.

Kipa wa Yanga, Shaaban Kado na winga wa Simba Salum Machaku walipambavyema onyesho hilo la uzinduzi ambapo walishiriki kwa pamoja na pamoja na wasanii wa kundi la THT na waigizajinyota wa filamu Tanzania, Aunt Ezekiel na Jacob Steven ‘JB’, nyota wa muziki waHip hop, Joseph Haule ‘Preofesa Jay’ na mwimbaji wa bendi ya African Stars‘Twanga Pepeta’, Janet Isinike ‘Janet Jackson’ na kushangiliwa kwa nguvu nawaalikwa kwenye sherehe hiyo.

Kwa mujibu wa Kavishe kampeni hiyo imetumia picha za Simba na Yanga,klabu ambazo zinadhaminiwa na bia hiyo.

katika kampeni hiyo pia wametumia lugha za mtaani, ambazo Kavishealisema ni fahari ya Tanzaniakwa mfano piga tarumbeta, neno linalowakilisha kunywa bia kwa kutumia chupamoja kwa moja na kula bata, yaani kula raha.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wada mbalimbali ambao walpata burudanimurua iliyoenda sambamba na kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager.

Kabla ya uzinduzi huo, Bia ya Kilimanjaro Premium Lager iliendeshasemina kwa waandishi mbalimbali wa habari za michezo na burudani ilikuwaelimisha kuhusu kampeni hii huku Kavishe akisisitiza kuwa wanahabari niwadau muhimu katika kupeleka ujumbe kwa umma hivi ni muhimu kwao kuelewakampeni hii na malengo yake

WANAOTEMBELEA KWA SIKU