Nahodha wa timu ya taifa akiwa na kocha wa taifa uwanja wa ndege
katikati mwenyekiti wa chaneta wakiwa na kocha wa taifa
mkurugenzi msaidizi wa idara ya michezo YASSODA akimkaribisha kocha uwanja wa ndege mara baada ya kuwasili
KOCHA wa timu ya TAIFA ya mpira wa pete , SIMONE MCKINNIS kutoka nchini AUSTRALIA amewasili nchini jioni ya jana na kutoa ahadi ya kuendeleza mchezo wa mpira wa pete hapa nchini katika kiwango cha kimataifa.
Muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JULIUS NYERERE, kocha MCKINNIS amewataka watanzania kuwa na subira wakati huu ambapo timu hiyo inajiandaa na mashindano ya Afrika yatakayofanyika kuanzia jumapili hii nchini AFRIKA KUSINI pamoja na kufanikiwa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa mpira wa pete zitakazofanyika mwakani nchini NEW ZEALAND
Kocha MCKINNIS anakuja nchini kufuatia ahadi iliyotolewa na Rais JAKAYA KIKWETE mapema mwaka huu ambapo kocha huyo atakuwa akipokea mshahara wa zaidi ya shilingi millioni 5 kwa mwezi kwa mkataba wa miaka MIWILI.
Kocha huyo kabla ya kuja nchini amekuwa mkurugenzi wa taasisi ya michezo nchini AUSTRALIA na pia amekuwa kocha mkuu wa netiboli katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 ya AUSTRALIA,nafasi ambazo zote amejiuzulu kabla ya kuja hapa nchini.






0 maoni:
Post a Comment