Wednesday, February 1, 2012

AIRTEL MZUKA DROO MHUDUMU WA STATIONARI AIBUKA MSHINDI WA MLIONI 50 YA AIRTEL

Mhuduma wa Stationari Magomeni aibuka mshindi wa mlioni 50 ya Airtel MZUKA
Mshindi wa pili wa million 50 katika promosheni ya Mzuka wa Airtel apatikana.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Jana iliendesha draw
kubwa ya pili ya kutafuta mshindi wa milioni 50/TZS iliyofanyika jana
usiku Majira ya saa mija na nusu na kurushwa live katika kituo cha
television cha ITV na kushuhudiwa na watanzania wengi ambapo Bi Halima
Omary Issa mkazi wa Magomeni Makanya aliibuka  mshindi wa kitita hicho
cha shilling million 50 pesa tasilimu.
Bi Halima Omary mwenye umri wa miaka 26 aliyeajiriwa kama mfanyakazi
wa stationary alisikika kuwa mwenye furaha iliyozidi kifani pale
alipopigiwa simu na Meneja uhusiano wa kampuni ya Airtel Bw Jackson
Mmbando na kupewa habari njema ya kuwa mshindi wa pili wa droo kubwa
na kujishindia million 50 pesa taslimu.
Katika maojiano na mshindi huyo yaliyofanyika kupitia televisheni ya
ITV live bi Halima Omari alisikika akisema “namshukuru sana mungu yani
sewezi kuamini nilishiki sana promosheni hii na nashukuru sana kuibuka
mshindi katika promosheni ya hii ya Airtel”
Akiongea kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel meneja
Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando “kupitia promosheni hii kabambe
tayari tumempata mshindi wetu wa droo kubwa yapili ya milioni 50 TZS
ya MZUKA lakini bado tumebaki na zawadi nyingi za simu mpya za kisasa
za sumsung tablet pamoja na muda wa maongezi na pia  mwisho wa mwezi
wa pili tutampata mshindi wa droo ya tatu wa milioni 50/-TZS ya
promosheni hii ya MZUKA”
Pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru watanzania na wateja wa Airtel
kwa kuendelea kutumia huduma za Airtel na kushiriki katika promosheni
hiyo,
Promosheni ya Mzuka inaendeshwa na Airtel kwa kipindi cha miezi mitatu
mfululizo ambapo ilizinduliwa rasmi mwishoni mwa mawka jana desemba
hadi mwishoni mwa februari mwaka huu 2012.
Zawadi kabambe wanazojishindia wateja kila siku ni pamoja na simu aina
ya Samsung, Muda wa maongezi, wakati washindi wa wiki wanajishindia
Samsung ipad, na washindi wa kila mwenzi pesa taslimu shilling million
50
Promosheni ya mzuka wa Airtel bado inaendelea hadi mwisho wa mwenzi wa
februari ambapo  zawadi mbalimbali zinaendelea kutolea na droo kubwa
ya mshindi wa tatu itachezeshwa mwishoni mwa mwenzi huu.
Kujiunga ni bure tuma ujumbe wenye neno “Mzuka” kwenda namba “15565”
na ujipatie nafasi ya kuibuka kuwa moja kati ya washindi.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU