Thursday, June 13, 2013

NBC YAZINDUA AWAMU YA PILI YA PROMOSHENI YA HIJA KWA WATEJA WAKE.

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC na pia Mkuu wa Hazina wa Benki hiyo, Pius Tibazarwa (wa pili kushoto),  Mkuu wa Kitengo Huduma za Kibenki kwa kufuata sheria za Kiislamu (NBC Islamic Banking), Yassir Masoud (kulia),  Mkuu wa Huduma za Rejareja, Mmoloki Legodu (wa pili kulia) na Naibu Mufti, Ali Muhidini Mkoyogore wakizindua promosheni ya pili ya Hija ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam leo.
 Mkuu wa Kitengo Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu (NBC Islamic Banking), Yassir Masoud (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya pili ya Hija kwa wateja wake  jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC na pia Mkuu wa Hazina wa Benki hiyo, Pius Tibazarwa na Mkuu wa Huduma za Rejareja, Mmoloki Legodu.
Mmoja wa washindi wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Hija ya NBC, Hamisi Hamza Mwanga (kushoto) akizungumza kuhusu safari yao ya kwenda hija mjini Makkah ambayo yeye na mama yake walikwenda kwa gharama za NBC.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU