Monday, May 23, 2011

BENKI YA NBC YAZINDUA TAWI KAHAMA

 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Mstaafu, Dk. YohanBalele akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya NBC wilayaniKahama, Mkoani Shinyanga juzi.
        Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Mstaafu, Dk. YohanaBalele (kushoto) akipokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBCTanzania, Lawrence Mafuru kabla ya kufungua rasmi tawi la benki hiyo,wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga juzi. Katikati ni Meneja wa NBCKanda ya Ziwa, Godhard Hunja
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Mstaafu, Dk. YohanaBalele akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Tawi la Benki ya NBCKahama kabla ya hafla ya ufunguzi rasmi wa tawi hilo wilayani humoMkoani Shinyanga juzi. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo,Lawrence Mafur

Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa tawi               

      Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Mstaafu, Dk. YohanaBalele akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya NBC wilayaniKahama, Mkoani Shinyanga juzi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji waBenki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru.                            

       
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Mstaafu, Dk. YohanaBalele akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa tawi la benkiya NBC wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga juzi. Kushoto ni MkurugenziMtendaji wa benki hiyo, Lawrence Mafuru.

BENKI ya NBC imezindua rasmi tawi lake la wilayani Kahama na kuahidi kutoa huduma bora zaidi na kuongeza mtanado wake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Kahama Mkoani Shinyanga juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru alisema NBC anazindua tawi hilo ikiwa imejipanga vizuri katika kutoa huduma zitakazokwenda sawa na mahitaji ya wateja wao katika eneo hilko maarufu kwa biashara za kilimo, ufugaji na madini.  

Akizidi kubainisha hilo katika uzinduzi huo ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Mstaafu  Dk Yohana Balele mkurugenzi huyo alisema licha ya matatizo hayo ya kiuchumi NBC imeendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania ikiwa na rasimali zilizofikia Trilioni 1.5 hadi kufikia mwisho wa mwezi Machi mwaka huu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Brigedia Mstaafu Dk Yohana Balele akizungumza wakati akizindua tawi hilo alisema NBC haikukosea kuwekezaa katika mkoa huo wenye sifa nyingi katika suala zima la uwekezaji.

Akitoa mfano alisema mkoa huo hususan wilaya ya Kahama ni maarufu kwa kilimo cha pamba na tumbaku, ufugaji na pia shughuli za madini akiutaja mgodi wa madini ya Alimasi wa Mwadui kuwa wenye sifa ya kuwa na mwamba mkubwa wa madini hayo kuliko duniani kote.

"Biashara katika mkoa wa Shinyanga ni kubwa licha ya mazao, ufugaji na madini lakini pia tumejaaliwa na barabara zinazounganisha nchi jiraji za Rwanda, Burundi na Uganda ambayo wafanyabiashara wengi wamekuwa wakiitumia kupitishia biashara zao", alisema.

Aidha mkuu huyo wa mkoa Dk Balele alitoa wito kwa benki nyingine ambazo bado hazijafungua matawi katika mkoa huo kuchangamkia nafasi hiyo mapema kuwekeza katika mkoa huo ambao licha ya kuwa na idadi ya watu wengi kuliko mikoa mingine nchini lakini pia inashika nafasi ya nne kiuchumi katika kuchangia pato la Taifa.

Tawi la NBC Kahama ni la nne kufunguliwa katika mkoa Mkoa huo wa Shinyanga katika mtandao wa matawi 54 ya benki hiyo chini kote.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU