Jerryson Tegete wa timu ya mkoa wa Mwanza akijaribu kumpita beki wa timu ya mkoa wa Arusha wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya pili ya michuano ya kili Taifa Cup 2011 inayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Mwanza ilishinda 2-1 na kutinga robo fainali
Jerryson Tegete wa timu ya mkoa wa Mwanza akijaribu kumpita beki wa timu ya mkoa wa Arusha wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya pili ya michuano ya kili Taifa Cup 2011 inayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Mwanza ilishinda 2-1 na kutinga robo fainali.
MABINGWA Watetezi wa michuano ya Kili Taifa Cup 2010 timu ya Mkoa Singida (Kidai Shooting) imeaga mashindano hayo kwa kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa timu ya Ilala, katika mchezo uliyofanyika kwenye Uwanja sheikh Amri Abeid.
Dakika ya 12 ya mchezo Salum Mpakala, aliipatia Ilala goli la kwanza baada ya kupiga shuti la mbali lililombabatiza beki wa Singida Charles Msuka na kumalizia mpira huo wavuni.
Mchezaji Vedastu Kaunda, aliipatia Ilala goli la pili baada ya kupata pasi toka Said Ahmed aliichanganya safu ya ulinzi ya Singida n kufunga goli hilo, mpaka Ilala ilitoka kifua mbele kwa mabao 2-0.
Katika kipindi hicho kila timu iliweza kufanya mashambulizi kadhaa lakini safu ya ushambuliaji ya Singida ilionekana kukata tamaa mapema.
Dakika ya 59 Omar Matuta aliipatia Ilala goli la tatu ambalo lilidumu mpaka mpira unamalizika.Ilala itakutana na mshindi kati ya Arusha na Mwanza waliokuwa wanacheza saa 10.alasiri.
Mashindano ya Kili Taifa Cup yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kili manjaro Premium Lager na masuala ya habari kuratibiwa na Kampuni ya Executive Solutions.
0 maoni:
Post a Comment