Wachezaji Mbwana Samata na Patrick Ochan ambao Simba inataka kuwatumia kwenyemechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco hawana uhalali wa kuchezea timu hiyo.
Simba kupitia TFF ilitaka kufahamu kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kama inaweza kuwatumia wachezaji hao kwa vile Hati ya Uhamisho wa Kimataifa(ITC) kuichezea TP Mazembe bado haijatolewa.
Kwa mujibu wa CAF, hawawezi kuichezea Simba kwa vile tayari wameuzwa, hivyokutokuwa na sifa ya kuwa wachezaji wa timu hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 26(1) ya Kanuni za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sifa ya mchezaji kwa mujibu wa kanuni hiyo ni kuwa na leseni iliyotolewa nachama cha mpira wa miguu cha nchi yake, leseni ya CAF, awe anaichezea timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa kwenye ligi ya nchi husika na awe anaishi katika nchi ilipo timu anayoichezea.
U 23 v NIGERIA- MICHUANO YA OLIMPIKI
Mechi ya kwanza ya mchujo ya michuano ya Olimpiki kati ya timu ya Taifa yaTanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 23 dhidi ya Nigeria itachezwa Juni5 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku.
Tumepanga muda huo kwa vile uwanja siku hiyo utakuwa unatumika kwa ajili ya michuano ya riadha ya Kanda ya Tano Afrika ambapo itakuwa inafikia kilele. Kwa mujibu wa Chama cha Riadha Tanzania (AT) kufikia saa 8 mchana michuano hiyo itakuwa imemalizika, hivyo kupisha maandalizi ya mechi.
Mechi itachezeshwa na mwamuzi Sylvester Kirwa ambapo atasaidiwa na Peter Kiereini, Aden Marwa na Davies Omweno wote kutoka Kenya wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Sahilu Gebremariam kutoka Ethiopia.
0 maoni:
Post a Comment