Shirikisho  la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko madogo ya ratiba  ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh  Kaluta Amri Abeid ulioko mkoani Arusha kuwa na shughuli nyingine za  kijamii.
Kati  ya Septemba 7 na 8 mwaka huu, na Septemba 17 na 18 mwaka huu, uwanja  huo utatumika kwa shughuli za dini na mashindano ya riadha ya Safari  International Marathon. 
Mabadiliko  ya ratiba yanahusisha mechi zifuatazo na tarehe mpya zikiwa katika  mabano; Septemba 7 mwaka huu mechi namba 20- Oljoro JKT vs Azam  (Septemba 9), Septemba 10 mwaka huu mechi namba 22- Azam vs Simba  (Septemba 11), Septemba 11 mwaka huu mechi namba 26- Ruvu Shooting vs  Yanga (Septemba 10).
Septemba  17 mwaka huu mechi namba 38- Oljoro JKT vs African Lyon (Septemba 19),  Septemba 21 mwaka huu mechi namba 43- Kagera Sugar vs Oljoro JKT  (Septemba 22), Septemba 21 mwaka huu mechi namba 49- Ruvu Shooting vs  African Lyon (Septemba 20) na Septemba 24 mwaka huu mechi namba 54- Toto  Africans vs Oljoro JKT (Septemba 25). 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)




0 maoni:
Post a Comment