Saturday, June 30, 2012

WASANII WA BONGO MOVIE WATOA MSAADA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO TANGA


Mwenyekiti wa Wasanii wa Bongo Movie,Jacob Steven "JB" akikabidhi msaada wa vyandarua kwa Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga,pia Mwalishi wa Hospitali hiyo,Bi. Halima Msengi (kushoto) wakati wasanii hao walipotembelea hospitali hiyo na kujioneea hali halisi ya uhaba wa vyandarua katika baadhi ya wodi.Msaada huo umekabidhiwwa hospitalini hapo mapema leo asubuhi kwa hishani ya kampuni ya Bia Tanzania Kupitia kinywaji Chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.

 Mkurugenzi wa Sofia Productions na Mratibu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (BONGO MOVIE),Mussa Kisoky akitoa (pili kulia) akitoa maelekezo kwa Wasanii wa Bongo Movie wakati walipofika Hospitali ya Bombo,Jijini Tanga kwa lengo la Kutoa Msaada wa Vyandarua ikiwa ni sehemu ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria nchini.
Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga,pia Mwalishi wa Hospitali hiyo,Bi. Halima Msengi (kushoto) akipokea Vyandarua kutoka kwa baadhi ya wasanii wa Bongo Movie waliofika Hospitalini hapo leo.
Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Jacob Steven "JB" wakiwa kwenye picha ya pamoja na Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga.Wasanii hawa wametembelea Hospitali ya Bombo mapela leo asubuhi kwa ajili ya kukabidhi msaada wa Vyandarua katika hospitali hiyo,ikiwa ni sehemu ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria unaopoteza maisha ya watanzania wengi katika maeneo mbali mbali ya nchini.Msaada huo umekabidhiwwa hospitalini hapo kwa hishani ya kampuni ya Bia Tanzania Kupitia kinywaji Chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Mwenyekiti wa Wasanii wa Bongo Movie,Jacob Steven "JB" wakijadiliana jambo lenye furaha na Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania,Fimbo Butallah wakati walipotembelea Hospitali ya Bombo,Jijini Tanga.
Safari ya kuelekea Wodini.
Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga,pia Mwalishi wa Hospitali hiyo,Bi. Halima Msengi (kushoto) akiwaeleza jambo Wasanii wa Bongo Movie waliotembelea Hospitali hiyo leo.
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa wamezunguka kitanda cha Mmoja wa Mama aliejifungua watoto Mapacha katika Wodi ya Wazazi wa Hospitali ya Bombo Jijini Tanga mapema leo asubuhi wakati walipofika kutoa Msaada wa Vyandarua kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Kinywaji chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Wasanii wa Bongo Movie,Rich Mtambalike na Hatman Mbilinyi wakipatia Chandarua mmoja wa wazazi katika hospitali ya Bombo,Jijini Tanga leo.
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Mama Consolata Adam akimjualia hali Mmoja wa kina Mama waliojifungua leo kwenye wodi ya Wazazi,Ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Bombo,Jijini Tanga.
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa kwenye Wodi ya Wazazi Hospitali ya Bombo,Tanga leo
Mwenyekiti wa Wasanii wa Bongo Movie,Jacob Steven "JB" pamoja na Katibu wake,Issa Mussa "Claud" wakisaidiana kufunga chandarua kwenye moja ya kitanda cha kilichopo ndani ya Hospitali ya Bombo,jijini Tanga mapema leo asubuhi.
Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga,pia Mwalishi wa Hospitali hiyo,Bi. Halima Msengi (pili kulia) akiwaeleza jambo Wasanii wa Bongo Movie waliotembelea Hospitali hiyo leo.
Irine Uwoya (kulia) na Juma Mchopanga wakijiandaa kufunga chandarua.

Mmoja wa wasanii hao akiwa amembeba mtoto walipo tembelea wodini.

Wasanii wa Bongo Movie wakiwa na Meneja Masoko wa TBL,Fimbo Butallah (kulia) na Menena wa Kinywaji cha Grand Malt,Consolata Adam (pili kushoto) mara baada ya kukabidhi vyandarua hospitali ya Bombo jijini Tanga leo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU