Baada  ya kibali cha kuwazika nchini Tanzania wahamiaji toka Ethiopia  waliofariki ndani ya lorry walilokuwa wanasafiria kutolewa na Serikali  yao  ya  Ethiopia, Serikali ya Tanzania iliamua mazishi ya Raia hao wa Ethiopia  kufanyika Juni 29, 2012 Alasiri Mkoani Dodoma na Morogoro kwa baadhi ya  miili iliyokuwa imehifadhiwa hospitali ya Mkoa Morogoro na kazi  inayoendelea hapa ni ya uchimbaji wa makaburi.
 Vijana  84 wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakipita mmoja baada ya  mwingine wakitoa heshima zao za mwisho na kuwaaga ndugu zao kwa kutupa  udongo kwenye makaburi yaliyohifadhi miili ya wenzao waliopoteza maisha  katika tukio la kusafirishwa kwenye Lorry.
 Kijana  Chafamo Yosef (kulia) Muamiaji raia wa Ethiopia akitoa neno la shukrani  muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazishi kwa jinsi ambavyo wamepatiwa  msaada na serikali ya Tanzania tangu siku walipokutwa wametelekezwa,  miongoni mwa vitu alivyoahidi akifika nchini kwao Ethiopia ni kuwaelezea  watu wa Ethiopia kuwa walidanganywa na kusababishiwa matatizo makubwa  hadi baadhi yao kupoteza maisha lakini wao Mungu amewanusuru, wameona  nchi nzuri ya Tanzania, wamekutana na serikali nzuri iliyowahudumia kila  kitu, na wananchi wenye mioyo ya huruma na ukarimu.
 Raia  wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakiwa wameinamisha vichwa  vyao chini kuwaombea sala wenzao waliopoteza maisha wakati wa shughuli  ya mazishi.
 Safari  ya mwisho ya kuwasindikiza na kuwahifadhi katika nyumba zao za milele  wahamiaji 43 (21 Dodoma, 23 Morogoro) kutoka Ethiopia waliopoteza Maisha  ilihitimishwa kwa kazi ya kufukia makaburi iliyofanywa na vijana na  wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye mazishi hayo.
 Wahamiaji  hawa (walionusurika) wamekuwa watu waliozamia katika sala na maombi  baada ya kunusurika kifo ukizingatia baadhi ya wenzao walikufa katika  tukio hilo, kila baada ya chakula jioni wanapewa muda wa kufanya maombi.
 Wahamiaji kutoka Ethiopia walipatiwa kila aina ya msaada wa muhimu uliohitajika kwa wakati kama malazi, mavazi, chakula dawa,  matibabu ya kisaikolojia nk
 Mtoa  huduma ya kwanza wa Msalaba Mwekundu akimfunika mmoja wa wahamiaji  kutoka Ethiopia ambaye alikuwa na tatizo la maumivu kifuani.
 Vijana  walioandaliwa kwa ajili ya shughuli ya Mazishi wakishusha miili ya  Marehemu kwenye nyumba zao za milele (makaburi) ikiwa ni hatua za mwisho  za kuhitimisha safari ya mwisho ya kuwapumzisha watu hao waliopoteza  maisha.
 Vijana  Wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakilia kwa uchungu muda  mfupi baada ya miili ya Wenzao waliopoteza maisha kuwasili eneo la  maziko mjini Dodoma, jumla ya Waethiopia 43 walipoteza maisha ambapo 21  wamezikwa Dodoma na 23 Morogoro.
Vijana  Wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakiwa wamejipanga mistari  miwili wakionekana wenye huzuni muda mfupi baada ya kuwasili eneo  lililoandaliwa katika Manispaa ya Dodoma kwa ajili ya kuwazika wenzao  waliopoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha, jumla ya Waethiopia  43 walipoteza maisha ambapo 21 wamezikwa Dodoma na 23 Morogoro. Picha  zote na Jery Mwakyoma




0 maoni:
Post a Comment