Monday, March 18, 2013

MABONDIA PRINCE NAIDJALA NA SEKOTSWE NUSU WAZIPIGE KAVU KAVU

Immanuel "Prince" Naidjala

Mabondia Immanuel “Prince” Naidjala  wa Namibia and Lesley Sekotswe wa Botswana wamekutana leo katika mkutano wa waandishi wa habari. Kukutana kwao nusura kulete balaa kubwa baada ya mabondia wenyewe kuingia midadi na kutaka kuzipiga kavu kavu mbele ya vyombo vya habari 

Mkutano huo ulifanyika katika hotel ya Windhoek Country Club Resort ambayo ni moja ya Casino kubwa katika nchi ya Namibia. Vyombo mbalimbakl vya habari kutoka nchi za Afrika na Ulaya zilishiriki katika mkutano huo ambao wawili hao walitambiana kupeana mkongoto wa uhakika watakapokutana siku ya jumatano tarehe 20.


Mabondia hao wanakutana tena kesho tarehe 19 katika hoteli hii katika zoezi la kupima uzito kabla ya mpambano wao siku ya Jumatano ambayo ni siku ya Uhurru wa nchi ya Namibia. Viongozi wakuu wa serikali ya Namibia watahudhuria mpambano huo ambao ni mkubwa kuwahi kufanyika katika nchi hii yenye wakazi milioni mbili na ushee!

Naye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili jijini Windhoek leo akitokea nchini Ghana kulisimamia pambano hili la ubingwa wa “IBF International Title”

Rais Ngowi ametokea jijini Accra, Ghana ambapo alishughudia mabondia Richard Commey na Bilal Mohammed wakitoana jasho ambako Richard Commey aliibuka kuwa bingwa wa uzito mwepesi katika bara la Afrika.

Promota wa mpambano huo Nestor Tobias wa kampuni maarufu ya Sunshine Boxing Promotions ana uhakika wa mpambano huu kuvunja rekodi ya kuingiza watu wengi zaidi ya mapambano yote yaliyowahi kufanyika nchini Namibia.

Pambano hili litawakutanisha pia baadhi ya mabondia kadhaa katika mapambano ya awali ambako bondia Martin Haikali wa Namibia atakutana na Nelson Banda wa Zambia katika mpambano wa raundi 8.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU