Thursday, March 7, 2013

SAFARI LAGER YAFUNGA ZOEZI LA FOMU ZA PROGRAMU YA “SAFARI LAGER WEZESHWA”.

Jaji Mkuu wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa, Joseph Migunda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufunga zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager Wezeshwa Dar es Salaam jana.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufunga zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager Wezeshwa Dar es Salaam jana.Kulia ni Jaji Mkuu wa Programu hiyo, Joseph Migunda.


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imefunga  rasmi zoezi fomu za ushiriki wa programu ya wajasiriamali ya “Safari Lager Wezeshwa” msimu huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema kwamba zoezi la fomu za ushiriki wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa msimu huu tumelifunga rasmi leo. Baada ya hapa fomu hizo zitakusanywa kutoka katika vituo vyote na kukabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya kuzifanyia kazi.

Bw. Shelukindo aliendelea kufafanua kwamba programu hii ilipata mafanikio makubwa mwaka jana ambapo iliwawezesha wajasiriamali 54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na ruzuku za vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili. Alisema, “Upatikanaji wa fomu hizi ndio mwanzo rasmi wa safari kuelekea uwezeshaji wa wafanyabiashara wadogo wadogo kwa msimu huu. Safari Lager inatoa fursa kwa mara ya pili,  inawaletea wamiliki wa biashara nafasi ya kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa ruzuku nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika harakati za kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaojaza fomu za ushiriki na kufuzu vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia hasa ya Safari Lager ni kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia mafanikio katika kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii inayowazunguka”.Alifafanua kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo wadogo na sio wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya programu hiini kutoa hamasa kwa wajasiriamali kote Tanzania ili wajitahidi zaidi katika shughuli wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze kufikia ndoto zao. Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama fedha taslimu kwa watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi vitakavyomsadia mjasiriamali kulingana na kazi anayofanya.

Naye Bwana Joseph Migunda, jaji mkuu wa programu ya“Safari Lager Wezeshwa”kutoka taasisi ya TAPBDS, waratibu wa programu hii alisema kwamba baada ya fomu kukusanywa zitafikishwa kwao kwaajili ya kuzifanyia kazi ili kupata wahitaji sahihi kutokana na michanganuo yao jinsi walivyojieleleza na baada ya hapo watafutwa huko waliko ili kudhibitisha waliyoyaeleza kwenye fomu zao. Kama ilivyokuwa mwaka jana, washindi msimu huu wa pili watawezeshwa kwa kupatiwa elimu ya biashara na ruzuku za vitendeakazi mbalimbali kulingana na biashara zao.

Bwana Shelukindo alimaliza kwa kusema, “Tunatoa pongezikwa wajasiriamali kote Tanzania, Safari Lager inatambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu. Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba waendelee kuburudika na bia hii inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio unaofanya tunawawezesha wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia kamili, inayodhihirisha mabingwa!.
 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU