Friday, March 15, 2013

SAFARI NYAMA CHOMA MWANZA

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13d6dabd33ad64f7&attid=0.1&disp=inline&realattid=f_heb7si4o0&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1363365569016&sads=nb_OG0WKgOcqAPZZObxc4T78ARo 
Jaji Mkuu wa shindano la Safari lager Nyama choma, Douglas Sakibu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu vigezo watakavyovitumia kuamua nani mshindi wa shindano hilo kwenye ukumbi wa TBL Mwanza jana.Katikati ni Menej wa Bia ya Sfari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja Mauzo na usambazaji wa Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki.

Fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma Mkoa wa  mwanza zinatarajiwa kufanyika kesho katika Viwanja vya  Furahisha kwa udhamini wa TBL, kupitia Bia yake ya Safari Lager

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Mwanza Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alizataja Bar tano zilizofanikiwa kuingia fainali kuwa ni Victoria Prince ya CCM Kirumba,AR ya Nyakato,Shokeni ya Mkuyuni na Shooters ya Kirumba ndizo ambazo zitashindana na kumpata nani bingwa wa kuchoma nyama kwa mkoa wa Mwanza katika mashindano hayo yajulikanayo kwa “Safari Lager Nyama Choma Competition 2013”

Alisema Shelukindo fainali hizo zitasindikizwa na burudani ya Mziki kutoka kwa Bend ya Africana Music na wasanii mbalimbali ikiwemo ngoma za asili.
Shelukindo alisema, “Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma. Tumezingatia maombi ya washiriki mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji nyama ilitafanyika kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma”. Bwana Shelukindo aliendelea kufafanua kwamba, washiriki watapimwa ujuzi wao katika kutayarisha nyama choma za aina tatu; nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya kuku.
 
Kiongozi wa jopo la majaji ambao ni wataalamu maarufu nchini katika tasnia hii, bwana Douglass Sakibu alielezea kwamba majaji wataangalia kwa makini sana vigezo mbalimbali katika utayarishaji wa nyama choma. Alitaja baadhi ya vigezo hivyo kwamba ni usafi, vifaa vya kufanyia kazi, joto maalum la uchomaji nyama nk. Bwana Sakibu aliendelea kusema kwamba, “Tynawaomba wakazi wa Mwanza wajitokeze kuja kula nyama Bora na kushuhudia Bar bora itakayoshinda katika fainali hizo jumapili katika viwanja vya Furahisha
Nae Meneja Mauzowa na usambazaji wa Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki alizitaja zawadi kwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni moja,wa pili laki nane,watatu laki sita ,wanne laki nne na wa tano lai mbili.

Malaki alilisisitiza kuwaomba wakzi wa Mwanza wajitokeze kwenye fainali hizo
Washuhudie Bar bora kwa kuchoma nyama na kupata burudani bure kwani hapatakuwa na kiingilio chochote.
 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU