Monday, March 4, 2013

TANGA CEMENT WASHIRIKI KILIMANJARO MARATHON 2013

 Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya saruji Tanga, Mary Stefano Msemakweli (kushoto) na Modesta Mbiu (kulia) wakishiriki mbio za kujifurahisha za Vodacom Fun Run za kilomita tano za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2013 mjini Moshi juzi. Tanga Cement ilidhamini kituo cha maji na soda kwa ajili ya wakimbiaji hao.
 Mfanyakazi wa Kampuni ya Tanga Cement, Rehema Mtondoo (kulia), akimwagia maji ili kumpunguzia joto mmoja wa wakimbiaji wa mbio za Nusu Marathon za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2013 mjini Moshi. Tanga Cement ilidhamini kituo cha maji na soda kwa ajili ya wakimbiaji hao.
 Ofisa Mawasiliano wa Tanga Cement, Mtanga Noor (kulia) akigawa maji ya kunywa kwa baadhi ya wakimbiaji wa mbio na Nusu Marathon za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2013 mjini Moshi . Tanga Cement ilidhamini kituo cha maji na soda kwa ajili ya wakimbiaji hao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Saruji Tanga, Erik Westerberg  (kulia) na Meneja wa Kiwanda cha Tanga Cement, Injinia Ben Lema wakishiriki mbio za kujifurahisha za Vodacom Fun Run za kilomita tano za Kiimanjaro Premium Lager Marathon 2013 mjini Moshi jana.
Wafanyakazi wa Tanga Cement wakipasha viungo kabla ya kuanza kwa kindumbwendumbwe cha mashindano ya mwaka huu ya Kilimanjaro Premium Lager Kilimanjaro Marathon mjini Moshi.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU