Saturday, June 15, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UJUMBE WA CHAMA CHA UKOMBOZI CHA PALESTINA (PLO)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Ukombozi cha nchini Palestina (PLO) uliofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam jana Juni 14, 2013 kwa ajili ya mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Tayseer Khalid, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini Kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Juni 14, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO) na Asha-Rose Migiro wa CCM, wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo mara baada ya mazungumzo
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Tayseer Khalid, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam jana Juni 14, 2013. Kushoto ni Asha-Rose Migiro wa CCM na (kulia) ni Jihad Abu Zneid wa PLO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Asha-Rose Migiro wa CCM, baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam jana Juni 14, 2013. Katikati ni Jihad Abu Zneid wa PLO. Picha na OMR

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU