Monday, June 17, 2013

WAAMUZI KILIMANJARO WAGOMA KUCHEZESHA MKOMBOZI CUP 2013

Chama cha Waamuzi mkoa wa Kilimanjaro kimegoma kuwatumia waamuzi wake katika Michuano ya Mkombozi Cup inayoendelea katika Mji wa Moshi kwa kile kinachodaiwa malipo madogo, kudharauliwa na kuburuzwa na Kamati ya Michuano  husika.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Mkombozi Cup 2013 kwa vyombo vya habari mchana wa leo imesema waamuzi waliokuwa wakiwatumia ni kutoka FRAT mkoa wa Kilimanjaro ambao wamegomea kuendelea na kuchezesha mechi zilizobaki.

Hatua hiyo imekuja wakati ikiwa ni siku 4 tu baada ya michauno hiyo kuanza kutimua vumbi katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mandela(PASUA) na King George Memorial (SOWETO).
Sehemu ya Taarifa hiyo imesema kuwa mechi zilizokuwa zichezwe leo katika viwanja hivyo zimeahirishwa mpaka kesho Jumanne ya Juni  18, 2013.

Mechi hizo ni Nazareth dhidi ya Soweto katika uwanja wa Memorial (KUNDI B) na Best Maridadi dhidi ya Moshi United katika uwanja wa Mandela (KUNDI C).
Hata hivyo Kamati ya kuendesha michuano hiyo imesema inaendelea kutafuta waamuzi kutoka sehemu nyingine kwa ajili ya michuano hiyo.

JAIZMELALEO imefuatilia kwa kina na kutaka kujua mwaka ujao Mkombozi Cup 2014  itaweza kuwatumiwa waamuzi kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro na kwamba itawatumia waamuzi kutoka katika Wilaya ya Moshi pekee ili kuweza kukidhi uwezo wao.
Aidha imebainika kwamba waamuzi wa mchezo wa soka hawapatani wao kwa wao kiasi kwamba hakuna maelewana kati ya uongozi na waamuzi wenyewe.



MKOMBOZI CUP 2013


KUNDI A
KUNDI B
KUNDI C
KUNDI D
1
KITAYOSCE
KILI RANGERS
TPC
RELI
2
GREEN STAR
MVULENI
NEW GENERATION
SANGO
3
NYUKI FC
NAZARETI
BEST MARIDADI
KILI FC
4
GOLANI FC
SOWETO FC
MOSHI UTP
BOYS UTD

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU