Friday, June 14, 2013

WATANZANIA WAOMBWA KUWAPIGIA KURA WASHIRIKI WA BIG BROTHER

Watanzani wametakiwa kuwapigia kura nyingi kadri wawezavyo, wawakilishi wao katika shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’ linaloendelea nchini Afrika Kusini ili kuhakikisha wanaendelea kubaki ‘mjengoni’ wakipeperusha bendera ya taifa.

Wito huo, umetolewa na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya simu ya AirtelTanzania, inayodhamini shindano hilo,Jackson Mmbando, huku akiwatajawawakilishi hao waTanzania kuwa ni Feza Kessy  na Ammy Nando.

Mmbandoalisema kuwa, ili kuendelea kumbakisha Feza katikakinyang’anyiro cha BBA ‘The Chase,’ Watanzania wanapaswa kutuma ujumbe wenye jina ‘FEZA’ kwenda namba 15456,

ili kumuokoa mshiriki huyo aliyeingia mara mbili kikaangoni, tofauti na Nando(22), ambaye anafanya vizuri.

“Watanzania tuna kila sababu za kuwapigia kura wawakilishi wetu, iliwaweze kuwakilisha vema na kipaumbele zaidi kiwe kwa kumpigia Feza kwakuandika jina lake kwa herufi kubwa “FEZA” kisha kwenda kwa namba 15456,” alisema Mmbando.

Mshindi wa mwaka huu, atajinyakulia kitita cha Dola za 300,000 zaMarekani.Tangu shindano hilo lianze ni Mtanzania Richard, ndiye pekee aliyewahi kushinda shindano hilo.

Mashindanohayo yanayofanyika kwa mara ya nane, yanashirikishawashiriki 24 kutoka nchi 14za Afrika na watakaa ndani ya nyumba hiyo kwa siku 90, ambako kusalia kwao mjengoni kunategemea kura za watazamaji wa shindano hilo.

Katikahatua nyingine, Mmbando aliwataka Watanzania kuendelea kulipiahuduma zao zaDSTV kupitia Airtel money, kwani kuna kuna kitu cha ziada kinakuja kwa ajili yao.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU