Monday, October 3, 2011

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akizungumza kabla
ya kupo mfano wa hundi ya shs milioni 10 kutoka kwa Mshauri wa Mambo
ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja (kulia kabisa nyuma)
zilizotolewa na NBC kama sehemu ya mchango wake kununulia  gari la
kubebea wagonjwa wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict kilichoko Kitunda
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Kushoto ni Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la Songea, Norbet Mtega na kulia ni  Mama Mkuu wa
Shirika la Masista Wabenedictini, Sr. Maria Shukrani Mkonde.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki  (wa pili kushoto)
akizungumza na  Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Songea, Norbet
Mtega (kushoto) wakati wakitembelea jengo jipya la Kituo cha Afya cha
Mt. Benedict katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho ambako
Benki ya NBC kupitia Mshauri wake wa Mambo ya Habari, Redemptus
Masanja (kulia) ilikabidhi hundi ya shs milioni 10 zitakazotumika
kununulia  gari la kubebea wagonjwa wa Kituo hicho. Wa pili kulia ni
Sr. Maria Agnesia wa kituo hicho. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam jana.
Wacheza ngoma ya asili wakitoa burudani katika hafla ya uzinduzi
wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict hafla ambayo Benki ya NBC
ilikabidhi hundi ya shs milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa gari la
wagonjwa wa kituo hicho. NBC pia imefungua akaunti maalumu ili
kukusanya fedha zitakazotumika kukamilisha ununuzi huo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU