Sunday, October 23, 2011

UBALOZI WA BRAZIL WAWAKARIBISHA WATANZANIA KWENYE MAONYESHO YA KAPOEIRA RUSSIAN CULTURE

 Mwalimu wa Mchezo wa Kapoeira ambao ni utambulisho halali wa Utaifa wa Brazil Mestra Janja (katikati) akizungumzia kuanza kwa warsha ya mchezo huo nchini Tanzania itakayofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo kuanzia Saa 12 jioni ambapo umuhimu na faida za mchezo huo vitafundishwa. Kushoto ni Kapoelista Gabriel Limaverde na Kulia ni Kapoelista Paula Andreewitch.

Afisa Michezo na Utamaduni Ubalozi wa Brazil nchini Tanzania Lazaro Ngimba (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na warsha ya mchezo wa Kapoeira itakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mda wa siku mbili ambapo amesema leo warsha hiyo itaanza Saa 12 jioni na kesho ni Saa 8 mchana na baadaye Wanakapoeira watakutana Kituo cha Utamaduni cha Russia ambapo Watanzania Wake kwa Waume wamealikwa kushuhudia mchezo huo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU