Monday, May 7, 2012

MAHAKAMA YATUPILIA OMBI LA KUHAMISHWA KWA KESI YA LULU

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali ombi la Mawakili watatu wanao mtetea Muigizaji nyota wa Filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu (17) anayehusishwa na kifo cha Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, aliye fariki dunia Aprili 7 mwaka huu nyumbani SINZA Jijini Dar es Salaam kuwa ana muri mdogo hivyo kesi yake iendeshwe katika mahakama ya watoto..

Wakili KENETH FUNGAMTAMA alidai Mahakamani hapo kwamba kutokana na umri mdogo wa mtuhumiwa wanaiomba Mahakama itoe udhuru kwa mtuhumiwa Elizabeth kushitakiwa katika Mahakama ya watoto kwa kuwa ana umri chini ya miaka 18 pia kesi yake iwe INCAMERA

Kwa upande wake wakili wa Serikali Elizabeth Kaganda alidai Mahakamani hapo kwamba hawakubaliani na ombi hilo hivyo wanaomba wachunguze umri sahihi wa Elizabeth kwa upande wao ili ukweli uweze kubainika.Kaganda amedai Mahakamani hapo kuwa umri wa Elizabeth unatatanisha kutokana na maelezo yanayotofautiana ya mtuhumiwa huyo alyoyatoa awali kwani alipohojiwa na Jeshi la Polisi alidai kuwa na umri wa miaka 17, pia majina yake katika cheti cha kuzaliwa ni Diana Elizabeth tofauti na linavyoandikwa katika kuwa Elizabeth Michael, upelelezi juu ya umri sahihi ni lazima.

Lulu amepandishwa kizimbani leo ikiwa ni mara ya tatu sasa ,mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam Augustina Mmbando, Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo na amerudhishwa rumande.

Hakimu Mmbando alitupilia mbali ombi hilo kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 196 kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za jinai hivyo ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 21 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU