Monday, May 7, 2012

41,733 WALIOSHUHUDIA MECHI YA SIMBA, YANGA

Watazamaji 41,733 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga iliyochezwa jana (Mei 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 VIP C, sh. 30,000 VIP B na sh. 40,000 VIP A. Watazamaji 36,980 walinunua tiketi za sh. 5,000 wakati 203 walikata za sh. 40,000.

Mechi hiyo ambayo ni moja kati ya saba zilizochezwa siku hiyo kufunga msimu wa 2011/2012 iliingiza sh. 260,910,000. Kila klabu ilipata sh. 62,646,395.85. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 39,799,830.51 wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilipata sh. 19,908,361.95.

Gharama za mechi kabla ya mgawo ni nauli ya ndani ya waamuzi na kamishna sh. 20,000, posho ya kujikimu kwa kamishna sh. 40,000, mwamuzi wa akiba sh. 30,000, gharama za tiketi sh. 8,539,950, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.

Mgawo wa uwanja ni sh. 19,908,361.95, gharama za mechi sh. 19,908,361.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 9,954,180.97, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 1,990,836.19 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 10,467,324.78.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU