Immanuel "Prince" Naidjala
Mabondia Immanuel “Prince” Naidjala wa Namibia and Lesley Sekotswe wa Botswana
wamekutana leo katika mkutano wa waandishi wa habari. Kukutana kwao nusura
kulete balaa kubwa baada ya mabondia wenyewe kuingia midadi na kutaka kuzipiga
kavu kavu mbele ya vyombo vya habari
Mkutano huo ulifanyika
katika hotel ya Windhoek Country Club Resort ambayo ni moja ya Casino kubwa
katika nchi ya Namibia. Vyombo mbalimbakl vya habari kutoka nchi za Afrika na
Ulaya zilishiriki katika mkutano huo ambao wawili hao walitambiana kupeana
mkongoto wa uhakika watakapokutana siku ya jumatano tarehe 20.
Mabondia hao wanakutana
tena kesho tarehe 19 katika hoteli hii katika zoezi la kupima uzito
kabla ya mpambano wao siku ya Jumatano ambayo ni siku ya Uhurru wa nchi ya
Namibia. Viongozi wakuu wa serikali ya Namibia watahudhuria mpambano huo ambao ni mkubwa kuwahi
kufanyika katika nchi hii yenye wakazi milioni mbili na ushee!
Naye Rais wa IBF katika
bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili
jijini Windhoek leo akitokea nchini Ghana kulisimamia pambano hili la ubingwa
wa “IBF International Title”
Rais Ngowi ametokea jijini Accra, Ghana ambapo
alishughudia mabondia Richard Commey na Bilal Mohammed wakitoana jasho ambako
Richard Commey aliibuka kuwa bingwa wa uzito mwepesi katika bara la Afrika.
Promota wa mpambano huo Nestor Tobias wa kampuni
maarufu ya Sunshine Boxing Promotions ana uhakika wa mpambano huu kuvunja
rekodi ya kuingiza watu wengi zaidi ya mapambano yote yaliyowahi kufanyika
nchini Namibia.
Pambano hili litawakutanisha pia baadhi ya mabondia
kadhaa katika mapambano ya awali ambako bondia Martin Haikali wa Namibia
atakutana na Nelson Banda wa Zambia katika mpambano wa raundi 8.
0 maoni:
Post a Comment