Monday, March 18, 2013

VICTORIA PRINCESS BAR MABINGWA SAFARI NYAMA CHOMA MWANZA.

 Mpishi Mkuu wa Bar ya Victoria Princes, Joseph Swai akishangilia mara baada ya kutangazwa mshindi wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika viwanja vya furahisha mwishoni mwa wiki.
 Wacheza shoo wa Bendi ya Africana ya jijini Mwanza wakicheza wakati wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma yaliyofanyika katika Viwanja vya Furahisha mwishoni mwa wiki.
 Mpishi Mkuu wa Victora Princes, Joseph Swai akishangilia na kitita cha shilingi milioni moja mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Amina Masenza (kushoto kwake) ikiwa ni Mabingwa wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma 2013 Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika katika viwanja vya furahisha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja mauzo na usambazaji wa kanda ya ziwa , Malaki Sitaki na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Amina Masenza (kulia) akimkabidhi kitita cha shilingi milioni moja Joseph Swai wa Bar ya Victoria Princes mara baada ya kuibuka mabingwa wa fainali za mashindano ya Safariri Nyama Choma yaliyofanuika katika Viwanja vya furahisha mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
 Mpiga Bess wa Bendi ya Africana akionyesha manjonjo yake wakati wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma yaliyofanyika katika Viwanja vya Furahisha mwishoni mwa wiki.
Mchina ambaye hakutambulika jina lake akicheza wakati Bendi ya Africana inatumbuiza wakati wa fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma yaliyofanyika katika Viwanja vya Furahisha mwishoni mwa wiki.

VICTORIA PRINCESS BAR, wametwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma Mkoa wa Mmwanza, baada ya kuzigaragaza baa nne zilizotinga fainali ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari Lager.

Kwa kutwaa ubingwa huo katika fainali zilizofanyika juzi Jumapili kwenye Viwanja vya Furahisha, baa hiyo ilizawadiwa fedha taslim Sh milioni moja pamoja na cheti.

Nafasi ya Pili katika fainali hizo ilishikwa na, Runara Hoteli ya Nyakatoi na kuondoka na kitita cha Sh 800,000 na cheti, wakati Gemston  walishika nafasi ya tatu na kupata zawadi ya Sh 600,000 na cheti.

Walioibuka na nafasi ya nne ni baa ya AR ya Kilimahewa iliyozawadiwa Sh 400,000 na cheti, wakati baa ya Shooters ilishika nafasi ya tatu na kuzawadiwa Sh 200,000 na cheti.

Akizungumza kabla ya kumtangaza mshindi, Jaji Mkuu wa fainali hizo, Douglas Sakibu, alisema kuwa walitoa mafunzo kwa baa zote hizo juu ya mambo wanayopaswa kuzingatia katika uchomaji nyama.

Alivitaja vigezo walivyotumia kupata mshindi kuwa ni usafi wa mchomaji, vifaa na mazingira, maandalizi ya nyama kuanzia uchaguzi, uhifadhi wake na wa vifaa.

Vingine ni uchomaji na upangaji nyama, ladha na ulaini wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa ni fahari kubwa kwa TBL na bia ya Safari Lager kwa ujumla kufanikisha shindano hilo mkoani hapa kabla ya kuhamia mikoa mingine.

“Tulianza kwa kuwataka watu wapige kura kupendekeza baa zinazofaa kuingia katika shindano la nyama choma kwa mkoa huu wa Mwanza tukapata baa hizi tano zilizoingia fainali ambapo leo tutampata mshindi.

“Tunajua watu huwa wanakwenda katika baa na kula nyama hivyo tukaona ni vema tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama choma wapate nyama bora,” alisema.

Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Masenza, aliisifu TBL kupitia Safari Lager kwa kuandaa mashindano hayo, akisema kuwa serikali inatambua mchango wa kampuni hiyo katika kujenga uchumi wa Taifa kupitia tukio hilo na mengineyo kama mashindano ya Pool Safari Lager, Safari Wezesha na hata udhamini wao katika michezo mbalimbali kama soka na mingineyo.

“Mashindano haya ni mazuri kwani yanawajengea wateja wa nyama mazingira mazuri na salama katika kutoa huduma hii ya nyama choma,” alisema.

Alizitaka baa ambazo hazikufika fainali, kutokata tamaa na badala yake kujipanga kwa ajili ya mashindano ya mwakani, kwa kurekebisha yale waliyokosea mwaka huu.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU