Monday, May 7, 2012

MWANASHERI​A MKUU AFAFANUA UTEUZI WA WABUNGE NA MAWAZIRI WAPYA

Mheshimiwa RaisJakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu yaBaraza la Mawaziri. Katika uteuzi waMawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutokamiongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza. Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwambahatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwaMawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.

Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenyemaslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia,kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge.

Msingi waKatiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4)kwamba: “Mawaziri na NaibuMawaziri wote watateuliwa kutoka miongonimwa Wabunge”
Pili, nimamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e)yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwawatu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalauWabunge watano kati yao wakiwa Wanawake. Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.

Tatu, baadaya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbungeanakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada yakuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwana Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake yauteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitajikuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli zaBunge.

Katiba yanchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwaWaziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza. Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia nikwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ilampaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Raiskiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wakazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifukatika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwamasharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapohivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.

Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwandani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au NaibuWaziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba auSheria. Aidha, katika kutekelezamadaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele yaRais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokeauteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa. Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwakatika kikao cha Bunge kijacho.

Bila shakaufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayikoisiyokuwa ya lazima.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU