Sunday, May 6, 2012

SIMBA YAIRARUA YANGA MAGOLI 5-0

Mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akiwania mpira mbele ya Shadrack Nsajigwa wa Yanga katika mchezao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania inayomalizika leo.
Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimvisha Medali mtoto wa mchezaji Uhuru Selemani wa Simba.
Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma baada ya timu ya Simba kuifunga Yanga magoli 5-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar salaam katika mchezo uliokuwa ni wa kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa, huku ikiwa tayari ni mabingwa wapya wa ligi hiyo, Simba imefanikiwa kutunza heshima yake baada ya kuifunga Yanga magoli 5 kupitia wachezaji wake Emmanuel Okwi, goli la kwanza.
Goli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu , Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari  
Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe leo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi akishangilia goli mara baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza . PICHA NA FULL SHANGWE

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU