Kufuatia ushindi huo wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa
Taifa, umepeleea Yanga kutimiza pointi 56 na sasa inahitaji pointi moja zaidi
katika mchezo wake ujao dhidi ya Coastal Union ya Tanga ili kubeba ubingwa.
Pamoja na ushindi huo Yanga SC leo iliwapa burudani nzuri
mashabiki wake kwa soka maridadi ya kuonana kwa pasi za aina zote, ndefu na
fupi, tena kwa staili zote hadi visigino.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Orden Mbaga, hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Simon Msuva, ambaye alifunga kwa ustadi wa hali ya juu.
Kipindi cha pili, Yanga SC walirudi na moto zaidi na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi, yaliyofungwa na Hamisi Kiiza dakika ya 59 na Nizar Khalfan dakika ya 64. Kiiza alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na David Luhende, baada ya Nizar Khalfan kuchezewa rafu nje kidogo ya eneo la hatari.
Nizar yeye alifunga baada ya kuuwahi mpira uliogonga mwamba na kurudi baada ya Frank Domayo kuunganisha krosi ya Haruna Niyonzima.
0 maoni:
Post a Comment