Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Prof. Benno Ndulu, akisaini
mfano wa cheti cha Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la
kusimamia na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazozorotesha huduma za
fedha nchini. Wanaoshuhudia nyuma (katikati) ni Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kulia kwake
ni Malkia Maxima wa Uholanzi (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha Sada
Mkuya Salumu. Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa
Benki kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa
Huduma za Fedha, wenye lengo la Kusimamia na kutatua ufumbuzi wa
changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla hiyo imefanyika
leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es
Salaam.
Malkia Maxima wa Uholanzi, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha wenye lengo la Kusimamia na kutatua
ufumbuzi wa Changamoto zinazozorotesha huduma za fedha nchini. Hafla
hiyo iliyohudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki
Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, leo.
Malikia Maxima wa Uholanzi, akibofya kitufe kama ishara ya uzinduzi wa
Mpango wa Taifa wa Huduma za Fedha. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es
Salaam, leo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal (katikati) Malkia Maxima wa Uholanzi na Naibu Waziri wa Fedha,
Sada Mkuya Salumu, wakiwa wameshikilia Mpango wa Taifa wa Huduma za
Fedha baada ya kuzinduliwa leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya
Tanzania. Picha na OMR
Baadhi ya wadau wa Sekta za Fedha waliohudhuria uzinduzi huo
wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia, wakati
wa uzinduzi.
0 maoni:
Post a Comment