Thursday, May 26, 2011

MBEYA USO KWA USO NA MWANZA FAINALI

 Mchezaji wa timu ya mkoa wa Mbeya, Juma Mpola (kushoto) akimtoka bekiwa timu ya mkoa wa Kagera , Laurent James wakati wa mchezo wa RoboFainali ya pili ya michuano ya Kill Taifa Cup 2011 dhidi ya timu yamkoa wa Kagera uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha
 Kipa wa timu ya mkoa wa Kagera akidaka mpira huku mshambuliaji wa timuya mkoa wa Mbeya Gaudens Mwaikimba akijaribu kufunga wakati wa mchezowa Robo Fainali ya pili ya michuano ya Kill Taifa Cup 2011 dhidi yatimu ya mkoa wa Kagera uliofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha jana
                                     
Kipa wa timu ya mkoa Kagera akiruka juu kuokoa moja ya hatari wakatiwa mchezo wa Robo Fainali ya pili ya michuano ya Kill Taifa Cup 2011dhidi ya timu ya mkoa wa Kagera uliofanyika katika Uwanaja wa SheikhAmri Abeid Arusha jana.

TIMU ya Mkoa wa Mbeya imeingia hatua ya Fainali baada ya kuifunga timuya Mkoa wa Kagera kwa mabao 2-1,mchezo uliyofanyika kwenye Sheikh AmriAbeid uliopo mjini hapo.
Goli la lilipatikana dakika ya 24 ya mchezo lililofungwa na GaudenceMwaikimba baada ya kipa wa Kagera kumkwatua mchezaji Said Mtupa,eneo la hatari.Dakika ya 60 Themi Felix, ameipatia Kagera goli la kusawazisha baadaya kutokea patashika langoni mwa Mbeya ambapo kipa wa Mbeya aliudakampira na kumponyoka kumfika miguu mwa mfungaji.
Dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kutoka kwa goli 1-1 ndipozilipoongezwa dakika na dakika ya 93 ya mchezo beki wa timu ya Kageraalijifunga akiwa katika harakati ya kuokoa ndipo mpira uliponasa wavuni.

Mpaka dakika 120 zimelizika Mbeya imeungana na Mwanza kucheza hatua yafainali ambayo itachezwa Jumamosi na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu atapatikana Ijumaa.

Mchezaji Bora katika mchezo huo alikuwa George Charles,aliyejinyakulia kitita cha sh.100,000 kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinyaji chake Kilimanjaro.Ilala na Kagera zitacheza kesho Ijumaa ili kumpata mshindi wa tatu.
Mashindano haya yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitiakinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager na masuala ya habariyanaratibiwa na kampuni ya Executive Solutions.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU