Monday, May 23, 2011

RUVUMA OUT TAIFA CUP

 Kipa wa timu ya Mkoa wa Mbeya, Ivo Mapunda(wa pili kutoka) akijaribu kuokoa moja ya hatari wakati wa mchezo wa roboFaianali ya Tatu ya Kili Taifa Cup dhidi ya timu ya mkoa wa Ruvuma
 Mshambuliaji wa timu ya Mkoa wa Mbeya, Mwagane Yeya akiwa ameruka juu kuwania mpira wakati wa mechi ya robo fainali ya tatu ya mashindano ya Kili Taifa Cup katyi ya Mbeya na Ruvuma.
Kipa wa timu ya mkoa wa Mbeya Ivo Mapunda na mshambuliaji wa timu ya mkoa wa Ruvuma, Kassim Kilungo wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya Tatu ya michuano ya Kili Taifa Cup inayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.Mbeya ilishinda 3-2.

TIMU ya soka ya Mkoa wa Ruvuma jana imeaga mashindano ya Kili Taifa Cup baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-2 toka kwa timu ya Mkoa wa Mbeya Mapinduzi (Stars) mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Jijini hapa
Dakika ya 3 ya mchezo Gaudence Mwaikimba aliipatia Mbeya goli la kwanza kwa kupiga mpira wa shuti la mbali lililotinga wavuni.Mchezaji Juma Mpola aliipatia Mbeya goli la pili baada ya kufanyiwa kazi nzuri na wachezaji Said Mtupa na Steven Mazanda naye kumalizia mpira wavuni.

Mpaka mapumziko Mbeya ilitoka kifua mbele kwa magoli 2-0, katika kipindi cha pili Ruvuma ilifanya mashambulizi kadhaa na dakika ya 49 ilipata goli kupitia kwa mchezaji Ally Bilali baada ya kupata pasi toka kwa Kassim Kilungo
Mwaikimba aliipatia Mbeya goli la tatu baada ya kuipangua safu ya ulinzi ya Ruvuma na kupiga shuti kali lililomshinda Kipa wa Ruvuma Hamad Waziri. Dakika moja kabla ya mchezo kumalizika ruvuma Ally Bilali aliipatia timu yake goli la pili lililofungwa kwa njia ya Penati baada ya mchezaji wa Mbeya Jumanne Elfadhili alimkwatua mchezaji Ally Bilali katika eneo la hatari.
Mashindano haya yamedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager na masuala ya habari kuratibiwa na Kampuni ya Executive Solutions

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU