TIMU ya Taifa Vijana chini ya miaka 23 imetolewa katika hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Kili Taifa Cup baada ya kukubali cha kipigo cha mabao 3-1 mchezo uliyofanyika kwenye Uwanja wa sheikh Amri Abeid.
Magoli hayo yalifungwa kwa njia ya penati baada ya 90 kumalizika Mwamuzi Israel Nkongo, aliamuru zipigwe penati baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
Kipa wa timu ya Mkoa wa Kagera Msafiri Davo ndiye shujaa wa mchezo huo kwa kuweza kupangua penati tatu zilizopigwa na wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana na kupata penati mojaWachezaji waliokosa penati hizo ni Khamis Mcha,Issa Rashid na Salum Telela wakati aliyepata penati katika timu hiyo ni Awadh Juma
Wachezaji wa Kagera waliopata penati ni Ibrahim Hassan, Juma Nade na Themi Felix.
Mchezo kwa ujumla ulikuwa mkali baada ya wachezaji wa timu zote kufanya mashambulizi kadhaa na kufanikiwa kupata magoli 2-2 katika dakika 90 za mchezo.
Katika mchezo huo mchezaji Juma Abdul wa timu ya Taifa ya Vijana amejinyakulia kitita cha sh.100.000 baada ya kuibuka mchezaji Bora wa mchezo huo.
0 maoni:
Post a Comment