Wednesday, May 18, 2011

SIMBA v WYDAD KUCHEZA CAIRO



Mechi ya kutafuta timu itakayocheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca ya Morocco itachezwa Mei 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa Petrosport jijini Cairo, Misri. Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) liliamua mechi hiyo ya mkondo mmoja ichezwe uwanja huru(neutral ground).
Iwapo muda wa kawaida wa dakika 90 utamalizika kwa sare, mshindi atapatikana kwa mikwaju ya penalti. Wenyeji wa mechi (kwa maana ya kupokea timu na viongozi
uwanja wa ndege) ni Chama cha Mpira wa Miguu cha Misri (EFA)

Gharama nyingine zozote zitabebwa na timu husika kupitia vyama vyao-Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco (FRMF).
Kila timu itajigharamia usafiri wa kwenda Cairo, pamoja na gharama za malazi.
EFA imeombwa kusaidia timu zote katika maandalizi ya hoteli za kufikia
Gharama za maofisa wa mchezo (waamuzi na kamishna) ikiwemo usafiri na malazi
zitabebwa na klabu hizo kupitia vyama vyao (TFF na FRMF). Gharama zozote ambazo
EFA itatumia katika maandalizi ya mechi hiyo zitarejeshwa na TFF na FRMF.
Pia mapato yatakayopatikana kutokana na viingilio katika mechi hiyo, EFA
itayagawa nusu kwa nusu kwa klabu hizo kupitia vyama vyao vya mpira wa miguu-
TFF na EFA.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU