Msimu wa Tano wa michuano ya Copa Coca Cola kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 unaanza kesho (Juni 11 mwaka huu) katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani katika viwanja vinne tofauti.Uzinduzi rasmi wa michuano hiyo utafanywa saa 8 mchana kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi. Mikoa yote 28 ya Tanzania Bara na Visiwani inashiriki katika michuano ya mwaka huu.
Mechi maalumu ya uzinduzi itakuwa kati ya bingwa mtetezi Kinondoni na Dodoma naitaanza saa 10 jioni. Viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo ni Tamco na Nyumbu vya Mkoa wa Pwani, na Karume na Tanganyika Packers (Kawe) vya Mkoa wa Dares Salaam.
Siku hiyo ya uzinduzi pia kutakuwa na mechi kati ya Temeke na Ilalaitakayofanyika Uwanja wa Tanganyika Packers, Kigoma itapambana na Pwani kwenyeUwanja wa Nyumbu wakati Mjini Magharibi itaoneshana kazi na Morogoro katikaUwanja wa Tamco. Mechi hizo zitachezwa saa 2.30 asubuhi.
Ukiondoa mechi hizo rasmi za ufunguzi, kila siku kutakuwa na mechi mbili kwenyeviwanja vyote. Mechi ya kwanza itaanza saa 2.30 asubuhi wakati ya pili itachezwasaa 10 jioni.
Hatua ya awali inachezwa katika makundi manne ya timu saba saba ambapo nne zakwanza katika kila kundi ndizo zitakazoingia hatua ya 16 bora.
Fainali itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati waamuzi 20 ambao wanaumri chini ya miaka 17 wakiwemo wasichana wawili ndiyo watakaochezesha michuano hiyo.
0 maoni:
Post a Comment