Tuesday, March 5, 2013

AIRTEL YAONGEZA MPUNGA -AMKA MILIONEA

 
 
Kwa siku 60  zaidi ya wateja 580  wa Airtel kuibuka na Mamilioni hayo
·         Tuma shinda kwenda 15595 ili kujiweka kwenye ushindi
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeongeza muda wa promoshei yake kabambe ya AMKA MILIONEA pamoja na sambamba na kuongeza kiasi kikubwa cha MPUNGA ili wateja wake kuendelea kujizolea mamilioni zaidi

Meneja Uhusiano wa Airtel ametuhabarisha kuwa promosheni hiyo iliyodumu kwa siku 90 hapo awali na kufanikiwa kuzawadia  zaidi ya milioni 400 kwa wateja wameamua kuiendeleza ili wateja waendelee kufaidi zaidi

“promosheni inaendelea sasa! Kila mteja wa Airtel anaweza akashiriki kwa kutuma neno MILIONEA au SHINDA kwenda 15595 na ataunganishwa bure

Zawadi zimeongezeka kila siku kutakuwa na washindi 10 watakaojishindia mamilioni kama kawa!!!

AMKA MILIONEA itahakikisha kila siku kunawashindi 10 kushinda kila siku na watagawana jumla ya shilingi  3,000.000, kila wiki jumla ya shilingi milioni 6,000,000 zitashindaniwa na washindi 10 na kila  mwisho wa mwezi  mshindi wawili watashindania na kugawana kitita cha shilingi milioni 30 wakati milioni  50, 0000Tshs itaenda kwa mshindi mmoja mwisho wa promosheni hii.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU