Tuesday, March 5, 2013

BINGWA WA MASUMBWI NA BINGWA WA NGUMI NA MATEKE KUZIPIGA TANGA

Alan kamote mwenye rasta kulia akimuadhibu mmoja wa mabondia aliowahi cheza nao

 Bingwa wa kickboxing Hamis mwakinyo   atazipiga na bingwa wa taifa wa ngumi za kulipwa nchini uzito wa light weight kg 60 Said mundi wa Tanga katika pambano la raundi nane, pambano la kusindikiza ubingwa wa mabara wa WBF kati ya Alan kamote na Jumanne Mohamed litakalopigwa katika uwanja wa mkwakwani  jijini Tanga tarehe 17 mwezi huu.
Hamis mwakinyo ambae ni bingwa wa ngumi na mateke afrika mashariki na kati wa  WKN-AFRIKA(World kickboxing Network- Afrika) na ameshawahi kuchalenji ubingwa wa dunia nchini iran anatazamiwa kuzipiga na  Said mundi  ambae ni bingwa wa ngumi wa taifa katika mpambano wenye ushindani mkali na unaozungumziwa na wapenzi wengi wa masumbwi  mkoani Tanga. Kwa maelezo ya muandaaji wa pambano hilo promota ally mwanzoa anaeleza kuwa  mabondia  hao wamesharidhia makubaliano  na wameshasaini  makataba wa makubaliano wa pambano hilo. 
Akithibitisha hayo mbele ya Ibrahim kamwe kwa kumuonesha nakala za mikataba  iliyosainiwa na mwanasheria wake,amesema  pia kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi kwa  mabondia toka sehemu mbalimbali za  Tanzania hususani  Dar es salaam na anategemea kuongeza nguvu  za majaji wa mchezo huo toka nje  ya Tanzania ili  kuondoa malalamiko yoyote yanayoweza jitokeza

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU