Monday, March 4, 2013

SAIGON PUB, WAMETWAA UBINGWA WA MASHINDANO YA NYAMA CHOMA MKOA WA MBEYA

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13d34bd7cf6a09f5&attid=0.2&disp=inline&realattid=f_hdvfeh2c1&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1362424652214&sads=wrvu_eDp-mjZSjN6jJ-K5UAZDkM 
Mkuu wa Wilaya wa Rungwe Mkoani Mbeya,Chrispin Meela (kulia)akimkabidhi kitita cha shilingi milioni moja Mpishi Mkuu wa Bar ya Saigon, Joseph Aluta mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Iromba mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Mkurugenzi wa Bar ya Saigon, Ally Mohamed na Meneja Mauzo wa rejareja wa Mkoa Mbeya, Michael Myinga
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13d34bd7cf6a09f5&attid=0.1&disp=inline&realattid=f_hdvfeh2c0&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1362424648640&sads=VbVFkFJ1_33O5IR_OXkMqsQc1PA
Wafanyakazi wa Bar ya Saigon na mashabiki wakishangilia huku wakiwa wamembeba mpishi Mkuu wa Bar hiyo,Joseph  Aluta mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Iromba mwishoni mwa wiki.

SAIGON Pub, wametwaa ubingwa wa mashindano ya Nyama Choma Mkoa wa Mbeya, baada ya kuzigaragaza baa nne zilizotinga fainali ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari Lager.
Kwa kutwaa ubingwa huo katika fainali zilizofanyika juzi Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Ilomba, baa hiyo ilizawadiwa fedha taslim Sh milioni moja pamoja na cheti.
Waliokuwa mabingwa watetezi wa mashindano hayo mkoani hapa, New City Pub, walishika nafasi ya pili na kuondoka na kitita cha Sh 800,000 na cheti, wakati Mbeya Carnival walishika nafasi ya tatu na kupata zawadi ya Sh 600,000 na cheti.
Walioibuka na nafasi ya nne ni baa ya Nebana iliyozawadiwa Sh 400,000 na cheti, wakati baa ya Chabruma ilishika nafasi ya tatu na kuzawadiwa Sh 200,000 na cheti.
Akizungumza kabla ya kumtangaza mshindi, Jaji Mkuu wa fainali hizo, Douglas Sakibu, alisema kuwa walitoa mafunzo kwa baa zote hizo juu ya mambo wanayopaswa kuzingatia katika uchomaji nyama.
Alivitaja vigezo walivyotumia kupata mshindi kuwa ni usafi wa mchomaji, vifaa na mazingira, maandalizi ya nyama kuanzia uchaguzi, uhifadhi wake na wa vifaa.
Vingine ni uchomaji na upangaji nyama, ladha na ulaini wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa ni fahari kubwa kwa TBL na bia ya Safari Lager kwa ujumla kufanikisha shindano hilo mkoani hapa kabla ya kuhamia mikoa mingine.
“Tulianza kwa kuwataka watu wapige kura kupendekeza baa zinazofaa kuingia katika shindano la nyama choma kwa mkoa huu wa Mbeya tukapata baa hizi tano zilizoingia fainali ambapo leo tutampata mshindi.
“Tunajua watu huwa wanakwenda katika baa na kula nyama hivyo tukaona ni vema tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama choma wapate nyama bora,” alisema.
Alisema kuwa bia ya Safari Lager ina miaka takriani 36 na bado imeendelea kuwapo hadi sasa ambapo Mbeya ndio inayoongoza kwa mauzo ya bia hiyo miongoni mwa mikoa yoye ya Tanzania.
Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Crispin Meela, aliisifu TBL kupitia Safari Lager kwa kuandaa mashindano hayo, akisema kuwa serikali inatambua mchango wa kampuni hiyo katika kujenga uchumi wa Taifa kupitia tukio hilo na mengineyo kama mashindano ya Pool Safari Lager, Safari Wezesha na hata udhamini wao katika michezo mbalimbali kama soka na mingineyo.
“Mashindano haya ni mazuri kwani yanawajengea wateja wa nyama mazingira mazuri na salama katika kutoa huduma hii ya nyama choma,” alisema.
Alizitaka baa ambazo hazikufika fainali, kutokata tamaa na badala yake kujipanga kwa ajili ya mashindano ya mwakani, kwa kurekebisha yale waliyokosea mwaka huu.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU