Saturday, March 16, 2013

YANGA WAENDELEA KUTESA

 
 Bao pekee katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lililofungwa na Hamis Kiiza katika dakika 48, limeiwezesha timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, kuibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0, dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo huo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini. Kwa ushindi huo sasa Yanga imefikisha jumla ya Pointi 48, huku Azam wakiendelea kubaki katika nafasi ya pili wakiwa na Pointi 37, na Simba wakiwa na Pointi 34 wakiwa nafasi ya tatu. Katika mchezo huo wa leo Kipa wa Ruvu Shooting Benjamin Haule, alionekana kuokoa hatari nyingi zilizoelekezwa langoni kwake. Katika michezo ingine iliyochezwa leo, kati ya Mtibwa Sugar na Coastal Union, katika Uwanja wa Manungu, timu hizo zimetoka sare ya 1-0. 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU