Saturday, March 9, 2013

YANGA YAZIDI KUJISHINDILIA KILELENI BAADA YA KUICHAPA TOTO AFRICA BAO 1-0

 
Mshambuliaji wa Yanga, akitoana na mchezaji wa Toto Africa, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,leo. 

Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Mshambuliaji Nizar Khalfan, aliyeingia kuchukua nafasi ya Jerry Tegete, akitokea benchi katika dakika ya 78. 
 
Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Azam amelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Moro, mchezo uliochzwa kwenye uwanja wa Chamazi Mbagala jijini Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo sasa Yanga imefikisha jumla ya Pointi 45 na Azam iliyo katika nafasi ya pili wakiwa na Pointi 37.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU