Sunday, June 16, 2013

FASTJET MABINGWA CASTLE LAGER SOKA FEST BONANZA 2013

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=13f4bc4eecd4086d&attid=0.1&disp=inline&realattid=f_hhzvi2te0&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1371405120561&sads=t5hyzrL10f1Hc-TeD1nFhWZp7us 
 Mabingwa wa Bonanza la Castle Lager Soka Fest,Fastjet wakishangilia na Kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika Bonanza hilo lililofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

TIMU ya soka ya Shirika la Usafirishaji wa Anga Fastjet imetwaa ubingwa wa Castle Lager Soka Fest Bonanza 2013 lililofanyika jana Jumamosi kwenye viwanja vya Chuo cha Posta jijini Dar es Salaam baada ya kuifunga timu ya Infinity Communications mabao 2-1  katika mechi ya fainali.
Infinity Communications walianza kupata bao la kwanza kupitia kwa Rahim Shaaban huku Fastjet wakisawazisha kupitia kwa Kelvin Kessy.
Fastjet walipata bao la pili na kutwa ubingwa wa bonanza hilo lililofungwa na Ally Ruvu.
Kwa kutwaa ubingwa huo, Fastjet walikabidhiwa Kombe, medali za dhahabu, wakati mshindi wa pili Infinity Communications walipata medali ya fedha na wa mshindi wa tatu BMF waliapata medali za shaba.
Nafasi ya tatu katika bonanza hilo ilichukuliwa na BMF walioifunga  Alpha kwa penalti 3-1, baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.
Awali bonanza hilo lilifunguliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Ridhiwani Kikwete, ambaye alikuwa mgeni rasmi.
 Akizungumza wakati wa ufunguzi wa bonanza hilo, Ridhiwani alisema michezo ni afya na kuwataka wanamichezo hao kushiriki michezo mara kwa mara.
“Michezo inajenga afya zetu, mimi binafsi huwa nashiriki michezo, jambo hili ni zuri, nawatakia kila la kheri katika ushiriki wa bonanza hili,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo, alisema bonanza hilo hufanyika kila mwaka na kwa mwaka huu lilianzia katika mikoa ya Mwanza, Iringa na kumalizikia Dar es Salaam.  
“Mwaka huu bonanza hili limeshirikisha makampuni 16 na tunatarajia mwakani makampuni mengi zaidi yatashiriki kwani mwamko umekuwa mkubwa na tunawahimiza waendelee kuinga mkono kwa kuendelea kunywa Castle Lager,” alisema alisema.
Timu zilizoshiriki katika bonanza hilo ni Taswa FC, Fastjet, Infinity Communications, DSTV, TBL, NSSF, Police Dar, IPP, BMF, KCB Bank, Gelod, Coca Cola, Aim Group, Facebook, Stanbic bank na Alpha.
Bonanza hilo lilipambwa na burudani kutoka Kalunde band na African Stars band ‘Twanga Pepeta’.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU