Msemaji wa yanga louis sendeu
Klabu ya YANGA imekanusha uvumi uliosambaa juu ya kutimuliwa kwa wachezaji wake wawili MOHAMED MBEGU na ERNEST BOAKYE huku usajili wa mshambuliaji KENETH ASAMOOH kufanyika mwezi ujao.
Afisa habari wa YANGA LOUIS SENDEU amesema kuwa MOHAMED MBEGU ameondolewa kambini kutokana na utovu wa nidhamu na suala lake linachunguzwa na kamati ya nidhamu ya YANGA, kwa upande wa ERNEST BOAKYE anasumbuliwa na maumivu ya tumbo yaliyomtokea kabla ya mechi yao dhidi ya AZAMU FC na yuko hospitali anaendelea na matibabu
SENDEU amesema usajili wa mshambuliaji wa timu hiyo mghana KENETH ASAMOOH utafanyika katika dirisha dogo la usajili linaloanza NOVEMBA MOSI kwa kufuata kanuni na taratibu mpya za usajli za FIFA.
Kwa upande wa kocha wa YANGA KOSTADINI PAPIC, SENDEU amesema suala lake la mkataba mpya linakamilishwa na kwamba hajatimuliwa kuinoa klabu hiyo kama ilivovumishwa na baadhi ya VYOMBO vya habari
0 maoni:
Post a Comment