Monday, November 8, 2010

ALLY HASSAN AWA MSHINDI UPANDE WA WANAMITINDO

Ally Hassan -(Daxx) the winner - Swahili Fashion Week 2010 model of the year award
Emerging designer Competition Winner Subira Wahume and Mustafa Hassanali, orgnizer of Swahili Fashion Week
Sothern Sun Best dress guest winner - Swahili Fashion Week 2010, Isabel Radick and her partner.
 

Swahili Fashion Week kwa mwaka watatu sasa imemalizika katika viwanja vya Karimjee tarehe 6 Novemba 2010, Dar Es Salaam , Tanzania, ambapo imetoa burudani tosha katika Sanaa ya ubunifu wa mavazi, sambamba na monesho ya kibiashara
Swahili Fashion Week iliwaleta  pamoja wabunifu wa mavazi 24 kutoka nchi zinazoongea lugha ya Kiswahili, ambapo wamekonga mioyo ya wapenzi wa Sanaa ya mavazi kwa kuonyesha ubunifu wao katika kubuni mavazi ya aina mbalimbali kwa kutumia aina mbalimbali za malighafi na mapambo.
Kwa upande mwingine Swahili Fashion Week imetoa zawadi za aina nne tofauti katika usiku wake wa mwisho, miongoni mwa zawadi hizo ni pamoja na standi bora kwa maonesho ya biashara, zawadi iliyokwenda kwa Muzu Sulemanjee wa Art & Frame.

Kwa upande wa zawadi iliyotolewa na Southern Sun Hotel imekwenda kwa Isabel Radick, baada ya kuibuka mshindi wa gauni bora, ambapo atapata fursa ya kulala hotelini hapo katika chumba cha hadhi ya juu mwishoni mwa wiki. Isabel alivaa gauni lililobuniwa na Kikoromeo mbunifu wavazi kutoka Kenya.

 “Swahili Fashion Week mwaka huu pamoja na kuonesha mavazi ya wabunifu wenye majina, pia imetoa fursa kwa wabunifu wanaochipukia kuonesha mavazi lengo ni kuthamini na kukuza vipaji vyao, sambamba na kuthamini kazi kubwa zinazofanywa na  wanamitindo wanochipukia.” Alisema Mustafa Hassanali, Muandaaji wa Swahili Fashion Week.

Mwaka 2009 zawadi ya mwanamitindo bora ilinyakuliwa na Victoria Martin, ambapo cheo hicho kwa mwaka huu amekabidhi kwa Ali Hassan.

Katika mchakato mzima wa wabunifu wanaochipukia, Waheru alikuwa na safari ndefu mpaka kufikia ushindi, kutoka wabunifu 31 wanaochipukia walioingia katika sindano, hatime alifanikiwa kuingi nusu fainali na kua miongoni mwa washindi walioingi fainali, ambapo wote kwa pamoja walipata fursa ya kuonesha mavazi yao  na hatimae kuibuka mshindi, nafasi itkayomuwezesha kupata mfunzo ya ubunifu wa mitindo kivitendo  yatakayotolewa na mbunifu wa mavazi wa siku nyingi nchini Manju Msitta. Mshind wa  pili ni Zarina Suleiman na Grace Kijo amechukua nafasi ya tatu.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU