Monday, November 29, 2010

NOVEMBER 30 MWISHO WA KUTHIBITISHA USHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA TAIFA

ROSE MKISI KATIBU MSAIDIZI WA CHANETA.
Chama cha netiboli Nchini CHANETA kimesema kuwa  November 30 mwaka huu ndiyo mwisho wa uthibitisho wa mikoa ya TANZANIA BARA kushiriki kwenye michuano ya kombe la TAIFA litakalofanyika kuanzia tarehe 12 mwezi Desember mkoani PWANI.

 amesema kuwa mpaka sasa ni mikoa 11 tu iliyothibitisha ushiriki wao barua lakini baadhi ya mikoa hiyo haijalipa ADA ya ushiriki

MKISI amesema kuwa baada ya tarehe hiyo kamati ya utendaji itakaa na kujadili kuhusiana na mashindano hayo ambayo yanalengo la kupata timu ya taifa ya mchezo huo itakayoshiriki katika mashindano ya kimataifa.

Ametaja baadhi ya mikoa iliyolipa ADA ya ushiriki kuwa ni ILALA,TEMEKE,KINONDONI,MTWARA,MOROGORO,MBEYA na PWANI.


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU