MKE WA MAREHEMU ABOU SEMHANDO
Ndugu wakiwa msimbani
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa msibani.
MAZISHI ya mwanamuziki na meneja wa bendi ya TWANGA PEPETA, ABOU ALLY SEMHANDO aliyefariki usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya pikipiki unatarajiwa kuzikwa kesho huko MUHEZA, TANGA.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, ASHA BARAKA amesema kifo cha ABOU ni pigo kwake ,wanamuziki wenzake na jamii kwa ujumla kwani alikuwa ni kama injini ya maendeleo ya katika bendi hiyo
Mauti yalimkuta Marehemu SEMHANDO aliyezaliwa mwaka 1953, katika maeneo ya TANGI BOVU baada bendi hiyo kumaliza kazi zao walizokuwa wakifanya katika eneo la AFRICANA ambapo marehemu hakuambatana na wenzake na kuendesha pikipiki yake na ndipo alipogongwa na gari aina ya benzi na kusababisha kifo chake papo hapo.
Mwili ya marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya muhimbili jijini DSM ambapo kesho alfajiri utaagwa katika hospitali hiyo na baadae kusafirishwa hadi Tanga kwa mazishi.
0 maoni:
Post a Comment