Monday, December 20, 2010

UWANJA WA MICHEZO WAJENGWA KANISA NA SHULE TABATA KISUKURU


Juhudi za kuhakikisha kwamba maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa shughuli za michezo yanatumiwa kwa makusudi yaliyotarajiwa  zinaelekea kugonga ukuta maeneo ya TABATA KISUKURU jijini DSM baada ya moja ya uwanja wa mpira wa miguu kuanza kujengwa shule na  Kanisa Katoliki PAROKIA ya TABATA.

Mwenyekiti wa mtaa wa KISUKURU, ZITO KEA anasema tayari ofisi yake imepokea barua ya kuendelea kwa ujenzi huo kutoka ofisi ya Kanisa Katoliki KIGANGO cha KIMANGA,lakini  na wao serikali ya mtaa wameandika barua kuomba kusitishwa kwa ujenzi huo ili kunusuru hatma ya vijana wengi wanaopenda michezo.

Baba Paroko wa Parokia ya TABATA Padre CYPRIAN KAGABA amekiri kufanyika kwa ujenzi huo na ameahidi kutoa ufafanuzi wa suala hilo hivi karibuni.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU