mkurugenzi wa tff SUNDAY KAYUNI
Shirikisho la soka nchini TFF limemteua kocha wa zamani wa simba JAMHURI KIWELO maarufu JULIO kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, SERENGETI BOYS kinacho jiandaa kushiriki michuano ya CECAFA yatakayoshirikisha nchi za TANZANIA, KENYA na wenyeji RWANDA yatakayoanza kutimua vumbi DECEMBA 17 jijini KINGALI.
Akizungumza jijini DSM kaimu katibu mkuu wa TFF SUNDAY KAYUNI amesema SERENGETI BOYS itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya wenyeji RWANDA desemba 17 kabla ya kumaliza na KENYA DESEMBA 22.
KAYUNI pia amewaalika wenyeviti na makatibu wa vilibu vya ligi kuu kufanya mkutano siku ya jumamosi kwa ajili ya maadalizi ya michuano ya UHAI CUP ambayo yanashirikisha timu za vijana chini ya umri wa miaka 20 ya vilabu vya ligi kuu Tanzania bara ili kupanga tarehe ya kuanza kwa michuano hiyo.
wakati huo huo kayuni amevitangazia vilabu tisa vitakavyoshiriki fainali ya ligi daraja la kwanza ambayo fainali zake zitanza kutimua vumbi January 15 mwakani.
Vilabu hiyo kutoka kundi A TEMEKE UNITED,VILLA SQUAD, na Moro united,kutoka kundi B ni TANZANIA PRISONS,COASTAL UNION na MORAN FC wakati kutoka kundi C ni JKT OLJORO FC,POLISI MORO,RHINO RANGERS.
0 maoni:
Post a Comment