Msemaji wa YANGA SENDEU
Klabu ya YANGA kuteremka dimbani dhidi ya AFC LEOPARD ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kujipima nguvu utakaochezwa kwenye dimba la UHURU jijini DSM siku ya Jumapili.
Akizungumza na TBC jijini DSM hii leo Afisa habari wa YANGA, LUIS SENDEU amesema mchezo huo ni wa kujiandaa na michuano ya ligi kuu ya TANZANIA BARA itakayoanza January 15 mwakani na kombe la shirikisho.
SENDEU amesema baada ya mchezo huo wa siku ya JUMAPILI dhidi ya AFC LEOPARD ya KENYA, YANGA itakwenda ZANZIBAR kushiriki mashindano ya kombe la Mapinduzi ambayo yamepangwa kuanza kutimua vumbi JANUARI mbili mwakani.
SENDEU ameongeza kusema kwamba Yanga itacheza na timu inayoshiriki ligi kuu ya BRAZIL itwayo PARANA ENSE January tisa katika uwanja uwanja wa taifa jijini DSM.
0 maoni:
Post a Comment