Timu ya TANZANIA TAIFA STARS jana imekula mweleka wa magoli MATANO kwa MOJA dhidi ya wenyeji MAPHARAO wa MISRI katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo ukiwa ni mchezo wa kundi A kwenye dimba la CAIRO INTERNATIONAL STADIUM.
Hakika haya yalikuwa maumivu makali mno kwa watanzania, kipigo cha magoli MATANO kwa MOJA.
AL SAYED HAMDY alipachika magoli mawili kwa MISRI hiyo jana,huku magoli mengine yakifungwa na MOHAMED ABOUTRICA,ISLAM ALI na lile la kujifunga na mlinzi wa STARS-NADIR HAROUB ALLY CANAVARO.
BAO PEKEE la kufuta machozi kwa TAIFA STARS limepachikwa wavuni na RASHID GUMBO.
Kwa matokeo haya STARS sasa wanashika mkia katika kundi A la mashindano haya kufuatia UGANDA nao hapo jana kuibuka na ushindi wa magoli MATATU kwa MOJA dhidi ya BURUNDI.
Katika mechi nyingine hiyo jana ikiwa ni mechi ya kundi B,KENYA imeibuka na ushindi wa goli MOJA kwa BILA dhidi ya SUDAN ukiwa ni ushindi wao wa kwanza katika kipindi cha miezi MINNE iliyopita.
Mechi nyingine zitafanyika JANUARY NANE siku ya jumamosi ambapo MISRI watavaana na UGANDA, TANZANIA na BURUNDI na JAMHURI YA KIDEMOKRASI YA CONGO dhidi ya KENYA.
Michuano hii itafikia tamati JANUARY 17 ambapo bingwa wake mbali na kombe la ubingwa pia atapata kitita cha paundi millioni 1 za MISRI sawa na shilingi millioni 250 za Tanzania,makamu bingwa akitia kibindoni paundi laki SABA za MISRI ambazo ni sawa na shilingi millioni 176 na wa tatu atapata paundi laki 6 za MISRI sawa na shilingi millioni 150.
0 maoni:
Post a Comment