Tuesday, January 11, 2011

UWANJA WA TAIFA KUTUMIKA KWA LIGI KUU TANZANIA BARA

                                Katibu mkuu wa TFF OSEAH na Mkurugenzi mkuu wa TFF SUNDAY KAYUNI wakiwa katika ofisi za TFF
Katibu mkuu wa TFF OSEAH pamoja na msemaji WAMBURA wakizungumza na waandishi wa Habari.
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limetangaza uwanja wa taifa jijini DSM kuwa utatumiwa na timu za ligi kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili baada ya kupata baraka kutoka kwa Wizara ya Habari, Utamaduni,Vijana na michezo.

Akizungunza na waadishi habari jijini DSM katibu mkuu wa TFF ANGETILE OSIAH amesema uwanja upo huru kutumiwa na timu za SIMBA, YANGA, AZAM FC, JKT RUVU na RUVU SHOOTING kama uwanja wao wa nyumbani kwa mechi za ligi kuu Tanzania bara mzunguko wa pili.

Vilabu vya SIMBA, YANGA, AZAM FC, JKT RUVU na RUVU SHOOTING vilikua vikitumia uwanja wa UHURU kama uwanja wao nyumbani kabla ya kufungwa kwa mategenezo na vikalazimika kutumia viwanja vya CCM KIRUMBA, JAMHURI MOROGORO na MKWAKWANI TANGA.

Wakati huo huo OSIAH amesema ni marufuku kuchezwa michezo ya kirafiki ya kimataifa kuanzia siku ya jumamosi ambapo mzunguko wa pili wa ligi kuu utakua umeanza ili kulinda kalenda ya TFF ambayo vilabu vyote na wadau mbalimbali wa soka wanayo nakala yake.


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU