Monday, January 17, 2011

UWANJA WA UHURU JIJINI DSM HURU KUTUMIKA KWA LIGI KUU TANZANIA BARA


Serikali imeruhusu kutumika kwa uwanja wa Uhuru kwa mechi za  duru ya pili ya ligi kuu soka Tanzania bara.

Afisa Habari wa shirikisho la soka hapa nchini BONIFACE WAMBURA amesema timu zote zilizokuwa zikiutumia uwanja huo kama uwanja wa nyumbani sasa zitaruhisiwa kuutumia tena ,ruksa hiyo ikivijumuisha pia vilabu vya SIMBA NA YANGA ambavyo vilikuwa tayari vimeruhusiwa kuutumia uwanja mkubwa wa TAIFA.

Mbali na SIMBA na YANGA vilabu vingine vilivyokuwa vikiutumia uwanja wa UHURU ni AFRICAN LYON, JKT RUVU, na RUVU SHOOTING.

Wakati huo huo TFF imesema mji wa TANGA utakuwa mwenyeji wa fainali za ligi daraja la kwanza zitakazoanza January 30 mwezi huu ,zitakazoshirikisha timu tisa, ambapo vilabu vinne vya kwanza vitapanda daraja na kushiriki katika msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU