Tuesday, January 25, 2011

WACHEZAJI THELATHINI VIJANA WAITWA KAMBINI

      
Makocha wa  timu ya Taifa ya vijana  chini ya miaka 23,20, 17  RISHARD ADOLF pamoja na JAMHURI KIHWELO wametangaza kikosi cha wachezaji thelathini wanaoanza mazoezi hapo kesho katika uwanja wa KARUME Jijini DSM.

Wakizungumza Jijini DSM makocha hao ADOLF na KIHWELO  wamesema wachezaji walioitwa wamezingatia nidhamu kiwango pamoja na ubora wa mchezaji.

Wachezaji wengine wa chini ya miaka ishirini wamechukuliwa wakati wa mashindano ya vijana ya vilabu vinavyoshiriki ligi kuu TANZANIA BARA yaliyomalizika hivi karibuni.

Makocha hao wamesisitiza wachezaji waliotajwa kwenye kikosi hicho wafike mara maoja kwenye mazoezi kuanzia hapo kesho.

Katika hatua nyingine kamati ya utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF iliyokutana January 16 Mwaka huu jijini DAR ES SALAA imepitisha majina ya wajumbe waliopendekezwa kuunda kamati ndogondogo  kwa kipindi cha mwaka 2011-2012 na kufanya mabadiliko makubwa katika kamati ya waamuzi ili kuongeza ufanisi.

Mabadiliko hayo  ni pamoja na LLOYD NGUNGA na JAMAL BAYSER waliokuwa wajumbe wa kamati hiyo ya waamuzi ambao sasa wamehamishiwa katika kamati nyingine tofauti kutokana na nyadhifa walizonazo katika vilabu.

NCHUNGA amehamishiwa katika kamati ya katiba , sheria na hadhi za wachezaji ilhali BAYSER anaingia katika kamati ya Habari na Masoko kama mjumbe.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa shiorikisho hilo ni kwamba STANLEY LUGENGE ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya waamuzi  wakati wajumbe ni OMAR KASINDE, RIZIKI MAJALA, JOAN MINJA na MOHAMED NYAMA.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo SHAIBU NAMPUNDE sasa ataongoza kamati ya ufundi na maendeleo.




                                     

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU