Thursday, January 27, 2011

WAZEE WA YANGA WATAKA WALIOFUKUZWA NA KUACHA KAZI YANGA WARUDI HARAKA

                          Wazee wa YANGA wakiwaza jinsi ya kurudisha amani katika klabu hiyo
                                      Wazee wa YANGA wakiwa na nyuso za huzuni
                     
Umoja wa wazee wa klabu ya YANGA umewataka viongozi walioachia ngazi na wale waliosimamishwa kurejea katika nafasi zao ili kuinusuru klabu hiyo ifanye vema katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya DEDEBIT ya ETHIOPIA

Wakiongea  katibu wa umoja wa wazee hao IBRAHIMU AKILIMALI, pamoja na wajumbe wa umoja huo MZEE HASHIMU MUHIKA na MZEE ABDALAH MOHAMED KIBARU wamesema  wanatarajia kuwakutanisha viongozi hao pamoja na wadhamini wa timu hiyo mara baada ya mchezo wa jumamosi  ili kusuluhisha machafuko yaliyopo katika klabu ya Yanga 

Kauli za wazee hao zinakuja ikiwa ni ndani ya wiki moja tayari  kumezuka kwa makundi ndani ya klabu ya YANGA baada ya kusimamishwa kwa meneja wa timu hiyo EMMANUEL MKANGALA, ikiwa ni pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo KOSTADIN PAPIC na katibu mkuu LAURENCE MWALUSAKO nao wakiachia ngazi kwa sababu tofauti

Klabu ya YANGA siku ya jumamosi inaingia dimbani kuumana na DEDEBIT ya ETHIOPIA katika mchezo wa kombe la shirikisho barani AFRIKA.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU